Woga wa Mtoto Kuachwa Peke Yake

Je, watoto wote wanapitia woga wa kuachwa?

Ndio, kwa kiasi fulani. Woga wa kuachwa ni hatua ya kawaida ya ukuaji wa kihisia kwa mtoto na inaanza watoto wanapoelewa vitu na watu vinapaswa kudumu katika maisha yao.

Katika baadhi ya hatua, watoto wengi wataonyesha woga /wasiwasi na kukasirika wanapotenganishwa na mzazi. Ni hali ya kawaida kwa mtoto asiyeweza kujitetea anapotengwa na mtu anayemlinda na kumjali kulia kwasababu ya woga.

Inatokea zaidi lini?

Watoto wanaanza kuonyesha dalili za uoga wa kuachwa mapema sana mwezi wa 6 au 7, ila kwa watoto wengi hali hii inakomaa kati ya miezi 10 mpaka 18 na kupungua miaka miwili.

Kawaida, uoga wa kuachwa unatokea pale unapoenda kazini. Mtoto anaweza kupata woga pia wakati wa usiku unapompeleka kitandani kulala, mara nyingi hali hii inapungua mtoto anapofika miaka miwili.

 

Jinsi gani naweza msaidia mwanangu?

Kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kumsaidia mtoto wako katika hali hii ya uoga wa kuachwa:

Andaa mazingira na mwanao kuzoea watu wengine: wakati wa kurudi kazini ukiwadia,itabidi umuache mtoto nyumbani. Ukirudi kazini jaribu kumuacha na watu ambao tayari anawafahamu kama bibi au babu yake, mdogo wako au dada wako wa kazi. Anaweza kupinga awali lakini atazoe pale anapozungukwa na watu anaowajua.

Andaa utaratibu: Amua utaratibu mzuri mfupi utakaoufuata kila wakati unapomuaga mwanao. Utaratibu unaojulikana kwa mwanao unasaidia kujenga uaminifu kutoka kwa mwanao na uwezo wake wakabiliana na woga wake.

 

Nimwandaaje mwanangu?

Fanya majaribio nyumbani: kabla ya kumuachia mtu mwanao, hakikisha umeshajaribu nyumbani ukiwa nae ili kujenga uaminifu kwa mtoto na kujifunza kila kitu kitakua sawa ukiondoka hata dakika moja au mbili, na utarudi. Kwa dhana hiyo mwanao atakua tayari kuachwa kwa mtu mwingine anayemfahamu. Akitambaa kuelekea chumba kingine kilicho salama muache aende na mpe muda kabla hujamfuata.

 

Siku zote muage mwanao vizuri:  mkumbatie na mpige busu kabla ya kuondoka. Mwambie unapoenda na utarudi saa ngapi, lakini kumbuka kumuaga mwanao kwa muda mfupi tu,na usirudi baada ya kumuaga. Usirudi, wala kukasirishwa pale unaomsikia mwanao analia baada ya kufunga mlango.

Mara unapoondoka, ondoka:  kurudi kumuangalia mtoto kutafanya hali iwe ngumu kwako, mwanao na msaidizi au mtu unayemuachia mtoto.

Kumbuka kumjaribu mwanao kwanza kabla ya kuanza kumkabidhi siku nzima mwanao kwa ndugu au msaidizi wako,unaweza kujaribu kumuacha saa moja na sio zaidi.

Woga wa kuachwa wakati wa usiku

Jitahidi kufanya masaa machache kabla ya kuenda kitandani yenye furaha na amani kwa mtoto, kwa njia hii itamsaidia mtoto kupata usingizi anaotakiwa bila kushtuka katikati ya usiku.

Mkumbatie, msome hadithi na kumuimbia nyimbo nzuri pamoja kabla ya kulala.

Ni sawa kumuendea mwanao pale anapolia mara baada ya kumuweka kitandani- itakusaidia wewe na mwanao wote kujua yuko salama. Hakikisha unafanya muda huo mfupi na usiomuhamasisha kuendelea kukusikiliza ili alale mara moja.

Ikiwa hakuna hata kimoja kimefanya kazi kumsaidia mwanao jaribu kutathimini njia unazotumia kumsaidia mwanao na wewe kukabiliana na woga wa kuacchwa. Hakikisha kuangalia mara ya pili mtu unayemuachia mwanao au sehemu (daycare) wakati mwingine mtu na sehemu unaomuacha mwanao vinaweza visiwe sahihi kwa mwanao.

Rudia mkakati wako wa kumuaga mwanao- fanya maagano yawe mafupi na usirudi kumuangalia anapoanza kulia mara unapoondoka.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.