Karibu AfyaTrack

Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto kwa Kiswahili.

Karibu AfyaTrack

AfyaTrack-Tovuti” pamoja na “AfyaTrack-App” ni huduma mtandao zilizoanzishwa nchini Tanzania kuwakomboa wanawake na watoto wakiwa kama kundi maalumu la afya kwenye jamii. AfyaTrack imedhamiria kutoa taarifa, ushauri na huduma za afya kwa jamii kuhusu ujauzito, mtoto na malezi bora kwa lugha ya Kiswahili. Maamuzi ya kutumua Kiswahili ni ili kuweza kuwafikia walengwa kwa lugha nyepesi na inayoeleweka ili kuleta mapinduzi ya uhaba wa taarifa sahihi za afya na zinazopatikana kwa wakati sahihi mtandaoni.

Piga namba hii kwa dharura ya afya, moto au polisi nchini Tanzania.

Makala Mpya

Jinsi ya kutunza kidonda baada ya kujifungua kwa upasuaji – caesarean section

Jinsi ya kutunza kidonda baada ya kujifungua kwa upasuaji – caesarean section
29Jan

Jinsi ya kutunza kidonda baada ya kujifungua kwa upasuaji – caesarean section

Hongera, Umeshindana na changamoto na kufanikiwa kujifungua salama kwa njia ya upasuaji, kwa sasa unahitaji kujifunza jinsi ya kujitunza ili…

Zifahamu Aina Mbalimbali za Uzazi wa Mpango
13Oct

Zifahamu Aina Mbalimbali za Uzazi wa Mpango

Uzazi wa Mpango ni Nini? Uzazi wa mpango ni maamuzi ya hiari ya mtu au wenza juu ya ni wakati…

Ninawezaje Kuongeza Nafasi ya Kupata Mtoto wa Kike au Kiume?
04Apr

Ninawezaje Kuongeza Nafasi ya Kupata Mtoto wa Kike au Kiume?

Je, moyo wako unafarijika kila uonapo nguo ya mtoto wa kike au kiume dukani au sokoni? Hakika unapata furaha ndani…

Ifahamu AfyaTrack App

Kwa wajawazito na walezi wa watoto nchini Tanzania, AfyaTrack App ni application ya kwanza na tegemezi kutoa taarifa, ushauri na makala maalumu za ufuatiliaji wa maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto wiki hadi wiki kwa lugha ya Kiswahili.

Maswali ya Mara kwa Mara

AfyaTrack App ni nini?
AfyaTrack App ni application ya simu za mkonnoni kama “Facebook” au “Instagram” inayokuwezesha kupata taarifa za maendeleo ya ujauzito au ukuaji wa mtoto wiki hadi wiki kwa lugha nyepesi ya Kiswahili. Unapopakua App hii na kuwa nayo kwenye simu yako una uhakika wa kupata taarifa na ushauri utakaoendana na umri wa ujauzito wako au mtoto wako kuhusu mabadiliko yako kimwili, mabadiliko yanayotokea kwa mtoto, lishe na vyakula, dalili hatarishi na vipimo maalumu, uhudhuriaji wa kliniki na chanjo husika, mazoezi na mapumziko, ukuaji wa mtoto na malezi bora na mengineyo mengi.
Application ya AfyaTrack inapatikana kirahisi sana. Kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa “Android” unachotakiwa kufanya ni kufungua app ya “Google Play Store” halafu unatafuta app ya AfyaTrack kwa kuandika maneno “AfyaTrack” kwenye sehemu ya kutafutia – search. Mara zote application itakayotokea ya kwanza ndio husika. Kisha unaipakua na hakikisha imeingia kwenye simu yako (Utahitaji kuwa na kifurushi cha kuperuzi mtandao kufanikisha hatua hii). Ukishafanikiwa kuiingiza kwenye simu yako hatua zinazofuata za kujiunga zinajieleza ukiifungua app.
AfyaTrack app inakupa uwezo wa kujiunga na huduma za ufuatiliaji wa maendeleo ya ujauzito wako au ukuaji wa mtoto wako. Ifahamike kwamba unaweza kujiunga na huduma moja kwa wakati mmoja. Unapoifungua app utapelekwa moja kwa moja kwenye sehemu ya kuingiza taarifa zako muhimu kama barua pepe, neno la siri nk. Ukifanikiwa kupita hatua hii, hatua inayofuata utaweza kuchagua huduma ya ufuatiliaji unayotaka kutumia, kati ya UJAUZITO au MTOTO. Ukichagua huduma ya Ujauzito utatakiwa kuingiza tarehe yako ya kwanza ya hedhi iliyopita ili application iweze kukupeleka moja kwa moja kuanza kupata taarifa za ujauzito kwa wiki uliyopo wakati huo. Ukichagua huduma ya Mtoto utahitajika kuingiza tarehe ya kuzaliwa ya mtoto husika ili uweze kupelekwa moja kwa moja kuanza kupata taarifa za ukuaji wa mtoto kwa wakati huo. (Kumbuka: Kwa sasa huduma ya ufuatiliaji ya ukuaji wa mtoto ni mpaka mtoto atakapofikisha mwaka mmoja pekee, tunaendelea kuongeza huduma hii ifike hadi miaka mitano na kuendelea)
BURE. App ya AfyaTrack haina malipo yoyote kuipakua au kujiunga kuweza kuitumia. Huduma hii inawezeshwa na mashirika mbali mbali yanayojali afya ya mama na mtoto kuifanya ipatikane bure bila malipo yoyote.

Vitengo

Taarifa

Pata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu afya ya mama na mtoto kutoka AfyaTrack Web na AfyaTrack App.

Jiunge na huduma zetu za ufuatiliaji wa maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa kupakua AfyaTrack App.

Huduma

Ushauri

Pata ushauri wetu wa afya ya mama na mtoto toka kwa Madaktari wetu

Pata mafunzo mbali mbali kwa kusoma makala zetu za afya zilizoandikwa na kupitiwa na wataalamu wetu wa afya.

Elimu

Utafiti

Shiriki na soma kuhusu tafiti mbali mbali tunazofanya na kushirikishwa na mashirika mengine.

AfyaTrack inakupa mwongozo na hatua za kuchukua pale unapopatwa na dharura.

Dharura

Ushauri wa Afya Toka kwa Wataalamu

Makala za kiafya zilizopo kwenye mtandao huu, pamoja na zile zilizopo kwenye application ya AfyaTrack zimeandikwa na kupitiwa na wataalamu wa afya. Hata hivyo ni vyema kutambua, ushauri unaoupata kwenye mitandao ni wa kuelimisha na kukupa uelewa wa taarifa mbalimbali za kiafya na sio vinginevyo. Unachokisoma kwenye mtandao huu hakitengui maamuzi ya daktrari ulipohudhuria au utakapohudhuria kituo chochote cha afya. Kwa maelezo zaidi soma:


1. Makala yetu ya sheria na taratibu za matumizi ya mtandao huu  Terms and Conditions
2. Makala yetu ya usiri wa taarifa zako Privacy Policy

Blog