AfyaTrack.com ni tovuti inayotoa taarifa, ushauri na huduma za kiafya mtandaoni. Katika ulimwengu wa sasa hakuna sababu ya mtu kutokuwa na uwezo wa kupata taarifa za kiafya za uhakika, kiurahisi na katika wakati muafaka.
AfyaTrack-Tovuti pamoja na “AfyaTrack-App” ni huduma mtandao zilizoanzishwa nchini Tanzania kuwakomboa wanawake na watoto wakiwa kama kundi maalumu la afya kwenye jamii. AfyaTrack imedhamiria kutoa taarifa, ushauri na huduma za afya kwa jamii kuhusu ujauzito, mtoto na malezi bora kwa lugha ya Kiswahili. Maamuzi ya kutumua Kiswahili ni ili kuweza kuwafikia walengwa kwa lugha nyepesi na inayoeleweka ili kuleta mapinduzi ya uhaba wa taarifa sahihi za afya na zinazopatikana kwa wakati sahihi mtandaoni. Baada ya kufanya tafiti mbalimbali kwa muda mrefu za namna ambavyo huduma za kiafya zinaweza kutolewa mtandaoni, AfyaTrack imefungua tovuti rasmi itakayokuwa inakuletea moja kwa moja huduma hizi popote pale ulipo ukiwa umejiunga na mtandao. Pia unaweza kupata huduma hizi kwa kupakua app ya AfyaTrack kutoka Google Play (Android).
Ni kweli kwamba asilimia kubwa ya Watanzania kwa sasa wanatumia huduma nyingi za kimtandao, ikiwemo mitandao ya kijamii kama facebook, Instagram na whatsapp. Ni wakati muafaka sasa kutumia uwezo huu wa mtandao kujifahamisha na kujiweka katika uelewa mkubwa kuhusu afya ya jamii na hasa hasa afya ya wajawazito na watoto.
Sehemu ya kwanza inahusu utoaji wa taarifa mbalimbali za kiafya. Taarifa hizi ni za moja kwa moja na zitakuwa zinalenga makundi yote katika jamii kwa kuanzia na kundi maalumu la wajawazito na watoto.
Sehemu ya pili inahusu utoaji ushauri mbalimbali kuhusu makundi maalumu kwenye jamii. Ushauri huu ni wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya na utakuwa unapatikana kwa yoyote aliyejiunga na AfyaTrack Web au AfyaTrack App.
Sehemu ya tatu inahusu utoaji wa huduma za kiafya kwenye mtandao. AfyaTrack inatoa huduma za kimtandao kuwezesha watumiaji kufuatilia hatua kwa hatua ujauzito tangu wiki ya kwanza hadi kujifungua pamoja na ukuaji wa mtoto tangu kuzaliwa mpaka mwaka mmoja.
AfyaTrack ni tovuti pekee inayotoa taarifa, ushauri na huduma kwa afya ya mama na mtoto kwa Kiswahili. Programu ya AfyaTrack ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za ufuatiliaji wa kila wiki.
© 2024 AfyaTrack. All rights reserved. A part of Afya4All Group.