Wakati muafaka unaoweza kupata ujauzito

Muda gani ni muafaka kufanya ngono ili kupata mimba?

Muda muafaka zaidi kujamiiana ni kipindi ambacho dirisha la kizazi linapokua (fertile window- siku tano kabla ya yai kupevushwa na siku ya yai kupevuka), wazi,kwa kawaida huchukua siku sita kwa kila mwezi. Siku hizo ni kipindi ambacho mwili unaruhusu upevushwaji wa mayai.

Yai la mwanamke linaweza kuishi kwa siku moja tangu linapozalishwa lakini manii zinaweza kua hai kwa muda wa wiki ndani ya mwili wa mwanamke, hivyo kuna siku sita ambazo mbegu za kiume zinaweza kusubiri katika kipindi cha upevushwaji wa yai (window period) kwa mwanamke kwa ajili ya kukutana na yai.
Unawezekana kupata mimba ikiwa utafanya tendo la ndoa ndani ya siku hizi au siku ya upevushwaji. Hata hivyo, ni vigumu kutambua siku halisi au mbili tu kabla ya yai kupevushwa. Kwa hiyo ikiwa hutaki maisha yako ya mapenzi yaongozwe na kalenda,njia nzuri ni kufurahia tu tendo kila siku mbili au tatu.

Ikiwa unataka kuwa sahihi zaidi, hata hivyo, unahitaji kufanya kazi ya ziada wakati yai linapevushwa.  Wakati yai linapevushwa kwenye mzunguko wowote uliojitokeza unategemea:

  • Urefu wa mzunguko wako wa hedhi
  • Jinsi hedhi yako ilivyo kawaida

Mzunguko wa hedhi unaweza kuwa mfupi wa siku 21 au mrefu wa siku 40. Kwa wastani huwa ni siku 28.

Bila kujali muda mrefu au mfupi mzunguko wako, kupevushwa kwa yai kawaida hutokea siku karibia na siku ya 14 kabla ya kuanza hedhi yako ya pili. Ikiwa una mzunguko wa siku 28, kuna uwezekano yai kupevuka katikati ya mzunguko wako. Ikiwa una mzunguko mfupi, yai linaweza kupevuka ndani ya siku za mwisho za hedhi yako.

Urefu wa mzunguko wa wanawake wengi unabadilika zaidi ya siku saba. Ikiwa mzunguko wako hubadilika mwezi mmoja kwenda mwingine,upevushwaji unaweza kutofautiana kwa wiki katika mzunguko.

Ndiyo sababu ni bora kufanya ngono kila siku mbili hadi siku tatu katika mzunguko wako. Ni ya ufanisi zaidi kuliko kuelekeza jitihada zako siku unayohisi yai litapevushwa. Pia, kufanya tendo la ndoa kila siku mbili hadi siku tatu inaboresha manii ikilinganishwa na ngono ya kila siku.

 

Je, ninajuaje nitakapokua karibu na mzunguko?

Unaweza kufahamu wakati wa upevushwaji wa yai au usipate mabadiliko yoyote kipindi hicho. Ikiwa unafikiri kupata ujauzito, kuwa makini na mwili wako ili uanze kuzitambua dalili za kupevuka kwa yai. Hali hii huweza kutokea wiki tatu kabla ya mzunguko unaotarajiwa kufuatwa. Jaribu kutazama yafuatayo:

  • Kuongezeka uteute ukeni. Hii inaitwa ute wenye rutuba.
  • Usumbufu upande mmoja wa tumbo lako.
  • Kuhisi zaidi kufanya tendo la ndoa.

Moja ya njia rahisi ya kugundua siku zako za upevushwaji ni kuchunguza uteute wa ukeni kila siku. Mabadiliko hayo ni moja ya kitu rahisi kukufahamisha unakaribia mzunguko.

Je, vipindi vya hedhi visivyofanana hufanya iwe vigumu kupata ujauzito?

Mzunguko usio eleweka hauna maana kwamba uwezo wako wa kuzaa ni mdogo kuliko mzunguko unaoeleweka. Hivyo ikiwa mzunguko wako haueleweki au unachukua zaidi ya siku 36,ni muhimu kumuona mshauri wako wa afya.

Wakati mwingine, mzunguko usioeleweka husababishwa na hali kama vile ugonjwa wa tezi za kizazi (PCOS) na kifua kikuu. Hali hizi zinaweza kuathiri mfumo wako wa uzalishaji, hivyo ni bora kupata msaada mapema badala ya baadaye.

Kadri mzunguko wako unavokua mgumu ndivo uwezo wako wa kuzaa unakua mgumu.       Hivyo, jitahidi kuangalia kila siku mabadiliko ya ute unaotoka ukeni.Jaribu kukutana kimwili na mwenza wako siku mbili au zaidi za siku za ambazo ute umetoka. Au unaweza kugundua kwa kupitia njia rahisi ya kujamiiana wakati wa mzunguko wako.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.