Vidokezo 9 kukusaidia kupata ujauzito haraka zaidi

Unajaribu kupata mimba? Mabadiliko rahisi ya maisha ya kila siku yanaweza kukusaidia kuongeza nafasi ya kupata mimba. Tazama vidokezo hivi:

 

Hatua ya kwanza: Acha sigara

Uvutaji wa sigara unajulikana kupunguza nafasi ya kuzaa kwa wanawake na wanaume. Ni hatari pia kwa mtoto kama bado unavuta sigara na una mimba.

 

Hatua ya pili: Fanya mazoezi pamoja

Kuwa imara kimwili ni njia kubwa ya kuongeza nafasi ya kuzaa. Kama hujazoea kufanya mazoezi, anza kwa kujenga mizunguko ndani ya siku. Kwa mfano, unaweza kushuka kituo kimoja kabla ya nyumbani ili upate kutembea zaidi au kutumia ngazi badala ya lifti. Unaweza kujiunga na darasa la kucheza au kukimbia mchakamchaka pamoja.

 

Hatua ya tatu: Kula kwa afya

Chakula na uzazi vinahusiana. Mkilia milo yenye afya pamoja, mlo kamili, mnaweza kuongeza nafasi ya kupata mimba. Jaribu pia kutafuta ni vyakula  vizuri kwa wanaume na wanawake wanapojaribu kutafuta mtoto.

 

Hatua ya nne: Pumzika!

Kujaribu kupata mimba kunaweza kuchosha. Kwa bahati mbaya, kuwa na mawazo sana inaweza kufanya ngumu kupata mimba, hivyo jsribuni kuchukulia mambo kiurahisi. Jipatieni mda wakupumzika kwa kufanya masaji, mazoezi ya kupumua kwa kina au kufurahia milo ya usiku pamoja. Chochote kinachoweza kuwafanya mpumzike na kuwa katika hali ya utulivu.

 

Hatua ya tano: Acha pombe

Pombe inaweza mdhuru mtoto kama unakunywa saana baada ya kupata mimba,hasa wiki za kwanza kabla ya kugundua una mimba. Kunywa kwa kupitiliza kunaweza kupunguza nafasi ya kuzaa kwa wanaume. Hivyo, ni vyema wewe na mwenzi wako kuepuka pombe, au kupunguza kabisa, mara mnapopanga kutafuta mtoto.

 

Hatua ya sita: Epuka joto kali kwenye korodani (wanaume)

Wakati korodani zikipata joto sana, mbegu za kiume(manii) huteseka. Kukaa mda mrefu kutumia laptop kwenye mapaja, au kufanya kazi katika mazingira yenye joto zinaweza kuleta madhara katika utengenezaji wa manii. Inashauriwa uvaaji wa nguo za ndani(boxer) zenye kubana kunachangia matatizo ya uzazi, ingawa hakuna ushahidi mwingi kwa hili. Ikiwa una matumaini ya kuwa baba ni wakati mzuri wa kuweka laptop pembeni  na kuvaa nguo zenye kukupa uhuru.

 

Hatua ya saba: Chukua likizo pamoja

Mapumziko au wikiendi ndefu pamoja inaweza kuwasaidia kupunguza msongo wa mawazo, na kufurahia mapumziko pamoja. Kiukweli, baadhi ya wazazi wameapa mapumziko ya pamoja yenye nia ya kutafuta mtoto (conceptionmoon) ni njia kuu ya kupata mimba.

 

Hatua ya nane: Fufua nuru katika mapenzi

Kama imeshindikana kuenda mapumziko, au kupata likizo, jaribu njia nyingine za kufufua mapenzi. Baadhi ya wanandoa wengi wanahisi wanafanya mapenzi kujaribu kupata mimba. Kama hili ni jambo linalokukumba, jaribu kurudisha mwanga katika mapenzi yenu.

 

Hatua ya tisa: Fanya mapenzi(sex) mara kwa

Tunavyojua kufanya tendo la ndoa ni muhimu san! Ingawa inasaidia kujua ni lini yai litapevushwa, kufanya mapenzi mara mbili hata tatu  itakupa nafasi nzuri ya kupata mimba.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.