Utaratibu wa Muda wa Kulala Mtoto

Vitu vya msingi vitakavyosaidia kupata utaratibu mzuri wa kulala

Kitu cha muhimu ni wewe kurudia utaratibu huohuo kila usiku ili mwanao aweze kukubaliana nao na kujifunza. Ikiwa haupo nyumbani jaribu kufuata utaratibu huo kama inawezekana,itamsaidia mtoto kutulia katika mazingira yake mapya.

Utaratibu huu ujumuishe kukaa nae chumbani kwake zaidi, hii itamfundisha kuwa chumbani kwake ni sehemu nzuri.

Mara unapomuweka mtoto kitandani na kumfunika kumbuka kumbusu na kumtakia usiku mwema. Ikiwa atalia wakati unaondoka, mkumbushe utarudi baada ya dakika tano kumuangalia, baada ya dakika hizo kama hajalala rudia tena  na ondoka dakika tano tena.

Ni nini nijumuishe katika utaratibu wa kulala kwa mtoto wangu?

Hakikisha unamchagulia mwanao michezo na shughuli zitakazomsaidia mwanao kuwa katika hali ya utulivu zaidi ya kumsisimua. Zifuatazo ni baadhi ya vitu unavyoweza kufanya:

Muogeshe

Maji ya moto wakati wa kuoga yatakusaidia kumfanya mwanao awe mkavu na msafi, hii ni njia rahisi ya mwanao kulala. Sio watoto wote wanapenda kuoga, wengine wanasisimuka zaidi wanapooga,ni vizuri kumnawisha miguu na uso na kumuogesha asubuhi.

Mpige mswaki

Utaratibu wa mwanao ujumuishe kupiga mswaki. Ni muhimu kuanza tabia ya kupiga mswaki mapema ili ajifunze kuyaangalia meno yake vizuri kadiri anavyokua.

Mbadilishe nguo kabla ya kulala

Mbadilishe mwanao, nepi mpya au mkumbushe kwenda chooni(kama anaweza). Kisha msaidie kubadilisha na kuvaa nguo za kulala.

Cheza mchezo wenye utulivu naye

Tumia muda wako kucheza nae mchezo kama kadi au kutegua kitendawili (puzzle) kabla ya kulala. Watoto wakubwa wanapenda kucheza kadi au kutegua kitendawili,lakini wadogo wanapenda mcheko wa kujificha. Hakikisha mchezo usiwe mkubwa na kumsisimua mtoto sana.

 

Ongea nae

Iwapo mwanao anaongea au hajaanza kuongea, wakati wa kulala ni muda mzuri wa kuongea nae. Kama mwanao bado mdogo wewe utahusika kwenye kuongea zaidi, lakini bado atapenda kukusikiliza.

Ongea nae kuhusu chochote mlichofanya siku nzima yote, na amejisikiaje. Kama mwanao ni mkubwa muulize jambo zuri na baya lililomtokea siku hiyo, na pia mkumbushe asiwe na wasiwasi wowote. Hii itamsaidia kukabiliana na woga au hofu na badala yake atapata usingizi mzuri.

Msimulie hadithi

Hadithi zitamsaidia mtoto kukuza misamiati na kuongeza upendo wake katika kusoma na kusimulia hadithi. Kama unamsomea mwanao hadithi chagua vitabu vya watoto anavyopenda kila usiku. Anaweza kupenda hadithi moja na kurudia kila siku, usikasirishwe na kitendo hichi ni muhimu katika ukuaji wake.

Muimbie wimbo

Nyimbo nzuri za watoto wakati wa kulala ni njia nzuri ya kumfanya mwanao apotelee usingizini vizuri. Sauti yako nay a mwenzi wako ni moja ya sauti anazozipenda mwanao. Iliwezekana rekodi sauti yako ukiimba na kisha muweke asikilize ikiwa mtu mwinine atamuandaa kulala siku nyingine.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.