Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya saba
Mtoto wako bado ni kiinitete, kwa sababu ana mabaki ya mkia ndogo ambayo hupotea katika wiki chache zijazo. Lakini hicho ni kitu pekee ambacho kinakuwa kidogo. Moyo wa mtoto wako na ubongo vinakuwa tata zaidi, mikunjo ya ukope wake vinatengenezeka, ncha ya pua yake inaanza kuonekana. Mikono yake sasa inajipinda katika viwiko na kujikunja kidogo zaidi juu ya kifua chake ambapo moyo wake upo.
Dalili za ujauzito katika wiki ya saba
Unaweza usionekane au hata usihisi una mimba, lakini mji wako wa mimba unapanuka kuweza kumtosheleza mtoto wako anayekua. Hapo kabla mimba ilikuwa na ukubwa wa ngumi. Sasa ni kubwa kama kichane cha tunda la zabibu (balungi). Kadiri mfuko wako wa uzazi unavyokua, unaweza kuhisi maumivu ya tumbo (cramps) na pia kichomi tumboni isivyo kawaida.
Hakikisha unawasiliana na daktari wako kama unapata vichomi tumboni. Kuna baadhi ya dalili za mimba ambazo kamwe usipuuzie. Kama una vichomi na kutokwa na damu, tafuta msaada wa matibabu mara moja. Daktari wako, mkunga, au hospitali yako katika kitengo cha ujauzito (Antinatal Clinics) vipo kukusaidia wewe.
Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya saba
Katika kipindi cha mwanzoni cha mimba ni jambo la kawaida kujisikia kama una hisia (emotions) kali. Unaweza kujisikia ecstatic (kuwa na furaha) kwa kuwa na mimba wakati mmoja, na baadae kuwa katika machozi ukiwaza kuhusu kuwa mzazi mtarajiwa. Mambo ya kijinga na madogo yanaweza kukufanya ujisikie vibaya na mwenye hasira, lakini wewe na mpenzi/mwenzi wako ni vyema kujua kwamba ni kawaida sana kuwa na kununa wakati mmoja na furaha wakati mwingine na hasira pia wakati mwingine. Ni vyema kutambua kuwa utakuwa na mabadiliko ya hisia mara kwa mara.
Mchanganyiko wa kufurika homoni na wasiwasi kuhusu ujauzito na uzazi pia unaweza kusababisha ndoto za wazi au kukosa usingizi kabisa (insomnia). Jaribu kupumzika na kuchukua muda wa kurejea katika hali ya awali ya utulivu na amani. Haya yatakuwa mazoezi mazuri kwa miezi ijayo. Heka heka za hisia(emotions) zinaweza kuendelea katika kipindi chote cha ujauzito na hali kuwa vizuri baada ya mtoto wako kuzaliwa. Hivyo kubali kwamba utakuwa unajisikia na kuhisi tofauti baadhi ya wakati katika kipindi hichi.