Ujauzito Wiki ya 40

Jinsi mtoto wako anavyokuwa katika ujauzito wiki ya 40
Ingawa pamebana huko tumboni mwako, mtoto wako bado anaongezeka taratibu. Nywele zake na kucha zinakua ndefu.

toto wako anaweza kuzaliwa na kucha ndefu, na sio lazima kuzikata mapema mno. Kutumia gloves za watoto “mittens” katika mikono ya kichanga wako hulinda asiweze kukwangua ngozi yake.

Ni vigumu kutabiri ukubwa wamtoto wako wakati wa kuzaliwa. Hata hivyo, tunajua kwamba watoto wachanga wana uzito wa wastani wa kilogramu 3.3 (7.3lb).

Mifupa ya fuvu la mtoto wako bado haijaungana, ambayo inaruhusu kuingiliana kidogo wakati akipita katika njia ya mfereji wa kuzaliwa wakati wa uchungu. Kuwa na uhakika kwamba ni jambo la kawaida na kwa muda mtoto wako kuwa na sehemu laini juu ya kichwa chake kwa angalau mwaka wake wa kwanza.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 40
Usingizi katika hatua hii unaweza kutokuja kwa urahisi .Kama ni vigumu kwako kupata usingizi usiku, jaribu kulala kwa mito au hata katika viti vizuri.

Unaweza kupata usingizi wakati wa mchana pia. Pumzika kadiri uwezavyo kwani itakusaidia kuhifadhi nguvu itakayohitajika wakati wa kujifungua. Jaribu kutokuwa na wasiwasi kwa kutokupata usingizi mzuri usiku katika siku hizi. Unaweza kujisikia bado macho maangavu wakati wa mchana, lakini mtoto wakohataathiriwa na ukosefu wako wausingizi.

Muongozo kuhusu ujauzito wiki ya 40
Baada ya miezi ya kutarajia kujifungua, tarehe yako ya kujifungua imepitiliza na wewe bado ni mjamzito. Jambo hili linaweza kukusikitisha na kuleta jazba, lakini ni kawaida. Kama uvumilivu unaelekea kukuisha, inaweza kusaidia kujikumbusha mwenyewe kwamba tarehe yako yenyewe ya kujifungua hutokana na kukadiria. Katika wiki 40, daktari wako au mkunga hawezi kufikiria kwamba muda wako wa kujifungua umepita “overdue” mpaka wiki moja zaidi ipite.

Wamama watarajiwa wachache wana kile kinachoitwa mimba za muda mrefu, ambazo huchukua muda wa wiki zaidi ya 42. Mkunga wako atakuangalia kwa makini katika siku hizi za mwisho. Unapaswa kuwa unahudhuria kliniki ya wajawazito kila wiki kwa sasa. Kama ujauzito wako ulikuwa wa moja kwa moja na usio wa matatizo daktari au mkunga wako lazima akuanzishie uchungu baada ya wiki ya 41.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 40
Je marafiki na familia yako hukupigia, au kutuma ujumbe kwako kila siku ili kujua jinsi mambo yanavyokwenda? Kama inakuchanganya, waeleza kwamba utawasiliana nao wakati mtoto wako ni dhahiri anakaribia kuzaliwa na si kabla! Au labda utawajuza baada ya kujifungua kabisa.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.