Ujauzito Wiki ya 39

Jinsi mtoto wako anavyokua katika wiki ya 39
Siku kubwa uliyokuwa unaisubiria ipo karibu sasa na haitakuwa muda mrefu sasa kabla ya wewe kuwa na uwezo wa kumkumbatia mtoto wako. Lakini usiwe na wasiwasi kama ifikapo mwishoni mwa wiki hii bado hujajifungua. Ni asilimia nne ya watoto wanazaliwa katika tarehe wanayotarajiwa. Watoto wengi huzaliwa ama mapema au wanachelewa.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 39
Wiki chache za mwisho za ujauzito zinaweza kuwa ngumu kama unakabiliwa nakiungulia. Acha kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi au kula kwa wingi kwa mkupuo.

Je, unajisikia kama muda umeenda tangu mwanzo wa ujauzito wako? Kama ndivyo, basi kuwa tayari kwa ajili mabadiliko ya kasi. Hizi siku chache za mwisho pengine utazihisi kuwa ni nyingi zaidi kuliko miezi tisa iliyopita.

Unaweza kuwa na hisia tofauti na wasiwasi juu ya kujifungua kwako, au wasiwasi kwamba utapitiliza tarehe yako ya kujifungua. Madaktari wengi na wakunga husubiri muda wa siku 10 hadi siku 14 baada ya tarehe yako kabla ya kuridhika kwamba mtoto wake amepitiliza muda husika na kamua kukuanzishia uchungu.

Wakati huo huo, wewe na mpenzi wako mnaweza kujaribu kupunguza mawazo kwa kufanya mapenzi kidogo. Tendo la ndoa linaweza kuwa na manufaa katika kufanya uchungu kuanza. Hata kama haitafanya kazi, angalau ni jambo la furaha kujaribu!

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 39
Mkunga au daktari wako anaweza kufanya kitu kinaitwa “membrane sweep” ambapo ni ili kujaribu kufanya uchungu uanze kawaida. Kama huyu ni mtoto wako wa kwanza, uchungu wako unaweza kuwa wa polepole na wa muda mrefu. Lakini, kuna njia mbalimbali za kuongeza kasi ya uchungu, za asili na kwa msaada wa dawa au vifaa maalumu.

Kama mama yako anakuja kukaa wakati mtoto wako kazaliwa, basi ni vyema kuwa umepata msaada toka kwa mtu ambaye ana uzoefu na huduma za mwanzoni zinazohitajika baada ya kujifungua kwako na kwa mtoto wako.

Je una wageni wengi wanategemea kuja kumjua mtoto wako mchanga? Hii inaweza kuwa balaa. Hivyo usijisikie vibaya juu ya kuweka baadhi ya watu mbali kwa zaidi ya wiki moja au mbili. Au kwa kupendekeza kuwa waje tu kwa muda mfupi na kuondoka.

Jambo la kwanza la muhimu kwa sasa ni wewe na mtoto wako. Unatakiwa upate muda wa kupumzika na kupona. Pia ni wazo zuri kuzuia watu na marafiki wa karibu kumbeba mtoto katika wiki ya kwanza.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.