Ujauzito Wiki ya 38

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 38
Mtoto wako sasa yuko tayari kusalimiana na dunia. Katika hatua hii, mtoto wako bado anajenga safu ya mafuta chini ya ngozi yake kumsaidia kudhibiti joto la mwili wake baada ya yeye kuzaliwa. Viungo vyake vyote vimeshakamilika, ingawa mapafu yake yatakuwa ya mwisho kufikia ukamilifu wake.

Kutoka wiki hii na kuendelea, kiasi cha maji ya uzazi “amniotic fluid” katika mji wako wa mimba kimeanza kupungua taratibu, ingawa mwiliwako utaendelea kutengeneza maji mpaka mtoto wako kuzaliwa.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 38
Unaweza kuwa unajihisi mkubwa na mwenye wasiwasi wakati wa wiki hizi za mwisho. Jaribu kuwa na amani. Kuangalia filamu, kusoma kitabu ambachohakina uhusiano kabisa na ujauzito au watoto. Pia ukipata nafasi kutana na marafiki kwani ni vitu ambavyo ukishajifungua utashindwa kuvifanya.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wikiya 38
Wiki hii utakuwa unahudhuria kliniki yako kwa mara ya mwishokabla ya mtoto wako kuzaliwa, isipokuwa kama utazidisha muda wa kujifungua. Hivyo tengeneza orodha ya maswali yoyote ya dakika za mwisho unaweza kuwa nayo kwa mkunga au daktari wako. Unaweza kuwa na maswali kuanzia jinsi ya kukabiliana na uchungu mapemana ni aina gani ya vituliza maumivu vinapatikana, ikiwa ni pamoja na vidokezo juu ya njia ya asili ya kupunguza maumivu na mbinu za kunyonyesha mtoto kwa mara ya kwanza.

Kama mpenzi wako ana wasiwasi kuhusu kukuangalia ukipitia maumivu, mjikumbushe wenyewe kwamba uchungu wa kujifungua ni tofauti na maumivu ya kawaida. Si ishara kwamba kuna kitu kibaya. Badala yake, ni ishara kwamba mtoto wako yupo njiani anakuja na misuli ya uzazi inafanya kazi vizuri kumsaidia kuingia ulimwenguni. Kama una watoto wengine, angalia kwa mara nyingine mipango ya mtu atakayekuwa anawaangalia pindi wewe na mpenzi wako mnaelekea kituo cha afya kujifungua.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.