Ujauzito Wiki ya 36

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 36
Hongera! Mwishoni mwa wiki hii, ujauzito wako utakua umefikia muda kamilifu. Hii ina maana mtoto wako anaweza kuzaliwa siku yoyote kuanzia sasa. Watoto waliozaliwa kabla ya wiki 37 ni njiti au kabla ya muda “pre-mature” , na wale waliozaliwa baada ya wiki 42 ni baada ya muda “ post-mature” Watoto wote ni tofauti lakini kawaida wenye umri wa wiki 37 huwa na uzito wa 2.8kg.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 36

Unaweza kuanza kuhisi kuongezeka kwa shinikizo katika tumbo lako la chini na kutambua kwamba hatua kwa hatua mtoto wako anashuka. Hapa mtoto anashuka na kuanza kuingia kwenye nyonga kuelekea kwenye mlango wa uzazi “cervix”.

Habari njema ni kwamba mapafu yako na tumbo lako hatimaye hupata nafasi ya kujinyoosha kidogo, hivyo kupumua na kula kunakuwa rahisi zaidi.

Hata hivyo, unaweza kutambua kutembea kunazidi kuwa kugumu . Uzoefu wako wa kubeba mtoto wako tumboni unaanza kuhisi utofauti kabisa. Baadhi ya mama watarajiwa wanasema hujisikia kama mtoto wao anakwenda kuanguka nje. Jaribu usiwe na wasiwasi kwani hii haiwezi kutokea.

Unaweza pia kujisikia kama una haja ya kwenda kukojoa wakati wote, kadiri mtoto wako anavyosukuma kibofu cha mkojo wako. Jaribu kufanya mazoezi ya sakafu yako ya nyonga yanaweza kusaidia.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 36
Kadiri siku yako ya kujifungua inavyokaribia, utajuaje kwamba sasa mambo ndio yanaanze kweli kweli? Kwa sababu uchungu halisi unaweza ukaanza wakati wowote kuanzia sasa ni vyema kuwa na uhakika wa usafiri hadi kituo cha afya, hakikisha una fedha za kutosha kufanikisha safari hizi na manunuzi ya maji na vyakula vya dharura, kama kuna malipo utakayohitajika kuyalipia kwenye kituo cha afya pia jitayarishe vyema kifedha. Usisahau pia kuhakikisha simu yako ya mkononi inakuwa na chaji ya kutosha muda wote na salio la kutosha kuweza kuwasiliana kipindi cha dharura.

Kama unategemea kujifungua mapacha soma zaidi makala yetu kuhusu kujufungua watoto mapacha kutoka kwenye miongozo yetu.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.