Ujauzito Wiki ya 35

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 35
Mtoto wako amekuwa mkubwa sana kwenye mji wake wa mimba na ni msumbufu, unaweza kupata mateke machache katika mbavu! Mtoto wako ameshaota tayari kucha za mikono na miguu. Figo zake zimekamilika na ini lake linaweza pia kusafisha baadhi ya taka.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 35
Unaweza kuwa na hisia kwamba huna nafasi – mji wa mimba yako umeongezeka wigo kwa mara 1,000 zaidi ya kiasi chake cha awali na sasa upo chini ya mbavu zako. Kama ulianza ujauzito wako katika uzitowa afya unaweza kuongeza kati ya kilogramu 10 na 12.5 (22lb hadi 28lb) kwa sasa. Utakuwa hauongezeki uzito sana kuanzia sasa.

Kama nywele yako zimezidi kung`aa kuliko kawaida, zifurahie sana wakati huu kwani zitarudi kama awali muda si mrefu baada ya kujifungua. Wakati wa ujauzito, nywele yako inakuwa nzito, kwa sababu homoni huzuia kupotea kwa nywele kwa kawaida.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 35
Ikiwa umeanza likizo yako ya uzazi, chukua nafasi ya kupata wakati wa kupumzika mara kwa mara mchana. Ni nafasi ya kufanya mazoezi na mbinu za kupumua ulizojifunza.

Kwa nini usipate (pedicure)usafi wa miguu na kucha wakati umepata muda? Unaweza kugundua ni ngumu mno kufikia miguu yako sasa tumbo lako kubwa linakuzuia.

Una mawazo ni namna ganikujifungua kwako kutakavyokuwa? Ni vigumu kutabiri uzazi wa mtu yeyote utakuwaje, lakini kuna njia unaweza kujaribu kuweka udhibiti wa mazingira utakayojifungulia. Kwa mfano, kwa kuhakikisha kuwa wakati ukifika mazingira yako ya kujifungulia ni kama ulivyopanga, kuanzia hospitali utakayojifungulia, usafiri utakaoutumia, mtu wa karibu utakayekuwa nae na hata mkunga atakayekusaidia wakati wa kujifungua ni kama upendavyo .

Kama wewe ni baba mtarajiwa, jifunze kuhusu njia bora za kuwa mzazi mwenza. Soma ratiba ya uzazi na pata maarifa unayohitaji kujua juu ya siku ile kubwa ya mwenza wako kujifungua. Hii itakuondolea hofu wewe pia na kukufanya uwe na amani kwani utahitajika kuwa na msaada mkubwa kwa mama mjamzito na hasa baada ya kujifungua.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.