Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 28
Mtoto wako sasa anaweza kufungua macho yake na kuwa na ari ya kuelekeza kichwa chake kwenye chanzo endelevu cha mwanga mkali.Kucha zake zinatumbika, na tabaka/safu ya mafuta inaanza kujijenga chini ya ngozi yake akiwa anajiandaa tayari na maisha ya nje ya mfuko wa uzazi.
Kama wewe utapenda wazo la kuzungumza na mtoto wako wakati yeye bado angali ndani yako, basi kuimba na kumsomea ni njia nzuri ya kufanya hivyo. Njia za neva za masikio ya mtoto wako zimekamilika sasa. Usijali kama utahisikuwa na wasiwasi kuwasiliana na mtoto wako kwa njia hii. Sio kila mtu yupo tayari kufanya hivi, ila ni vyema kutambua kuwa mtoto wako tayari anasikia kila kitu unachosema.
Dalili za ujauzito katika wiki ya 28
Simuda mrefu umebaki kwa sasa. Uko katika miezi mitatu ya mwisho, ambayo itaenda hadi mwisho wa ujauzito wako, kwa kawaida wiki 40 au zaidi. Unaweza kumwonadaktari wako au mkunga wako mara nyingi zaidi kuanzia sasa. Si lazima kusubiri mpaka siku yako ya kliniki kama unataka kujadili kitu chochote, au una tatizo ni vyema kwenda au kuwasiliana na daktari mara moja.
Pengine hupendi unavyohisi. Unaweza kufikiri, “Nimekuwa mjawazito milele”, au labda ukahisi, “siko tayari kwa hili”. Hakika haupo peke yako. Kubadilishana ujuzi na wamama wajawazito wengine kwenye madarasa ya wajawazito yaweza kukusaidia na kukutuliza kimawazo.
Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 28
Kama wewe ni baba, unajisikiaje kuhusu kuona mpenzi wakoakienda kujifungua? Kujua nini kinatokea wakati wa uchungu ni njia nzuri ya kujiandaa kwa ajili ya tukio hili litakalobadilisha maisha yenu.
Wakati mwingine, mambo yanaweza yasiende sawa kama ilivyotarajiwa wakati wa uchungu na kujifungua. Mtoto wako anaweza kuhitaji msaada ili azaliwe. Ongea na daktari au mkunga wako kuhusu huduma mbalimbali juu ya kusaidiwa kuzaa na kuhusu upasuaji, ili uwe umejiandaa vizuri na kuweza kumsaidia mwezi au mpenzi kupitia taratibu zote kama itahitajika.