Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 25
Sasa mtoto wako ameanza kufanya harakati za kuanza kupumua, ingawa hakuna hewa katika mapafu yake. Ufahamu wake unaendelea kukua kwa haraka. Katika hatua hii, tafiti mbali mbali zinaonyesha watoto huitikia miguso na mwanga.
Ukimulika tumbo lako kwa tochi, mtoto wako atageuza kichwa chake, hii itaonesha kwamba kiini cha mfumo wa fahamu wa macho yake “optic nerve” kinafanya kazi vizuri.
Dalili za ujauzito katika wiki ya 25
Unaweza kuhisi haja ya kuweka miguu yako juu kidogo mara nyingi zaidi sasa na kupumzika mara kwa mara. Japokuwa uchovu unaweza kuwa unarejea, jaribu kukaa mchangamfu na mkakamavu. Kuogelea ni zoezi zuri kadiri tumbo lako linavyozidi kuwa kubwa. Maji yanaubeba uzito wako na kunyoosha mishipa yako. Kuogelea taratibu na kwa makini hufanyisha mazoezi mwili wako mzima.
Jaribu kutokufanya mazoezi yoyote karibu sana na muda wa kulala,kufanya mazoezi jioni kunaweza kusababisa wewe ikawa vigumu kupata usingizi.
Tukizungumzia kupata usingizi, tumbo lako linalokua linaweza kukusababishia wewe kukosa nafasi ya wewe kupumzika vizuri. Inapendekezwa kulala kwa ubavu wako badala ya mgongo wako kutoka miezi mitatu ya pili “second trimester”. Unaweza kutumia mito kama egemeo kusaidia tumbo lako katika kitanda.
Jaribu kupendelea mfumo mzuri wa mlo bora. Mahitaji ya chakula kwa mtoto wako ni makubwa zaidi katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito.