Ujauzito Wiki ya 24

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 24
Mtoto wako anaendelea kukua kwa kasi. Mwili wake unajaza na kuchukua nafasi zaidi katika mfuko wako wa uzazi lakini ngozi yake bado ni nyembamba na tete. Pamoja na haya mtoto wako ana uwezo mkubwa sana wa kuishi kama akizaliwa kabla ya siku zake kuanzia sasa.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 24
Unaweza kuanza kuona michirisi ya mvutano “stretch marks” juu ya tumbo lako, kwenye makalio na chini ya matiti.

Kupaka mafuta au krimu mbalimbali zinaweza kusaidia kulainisha ngozi na kukufanya ujisikie vizuri na kuondoa miwasho na ngozi kuwa kavu, lakini haitaweza kuziondoa alama hizi za michirizi ya mvutano wa ngozi “stretch marks”. Alama hizi za mvutano wa ngizi ni za kawaida katika hatua hii ya mimba na kuisha kwa alama hizi ni baada ya kujifungua.

Unaweza pia kugundua kwamba macho yako hayapendi mwanga mkali na ni makavu. Hii ni dalili ya kawaida kabisa kwa ujauzito. Kama macho makavu yanakusumbua sana ni vyema kumuona daktari wako au daktari wa macho. Matibabu au dawa ambazo unaweza kununua katika maduka bila mwongozo mzuri kutoka kwa daktarizinaweza zikawa hazifai wakati wa ujauzito.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 24
Ni vyema kuanza maandalizi mapema. Kama mwenza wako yupo ni vyema kuanza kuzungumza pamoja kuhusu namna mtakavyoshirikiana pamoja katika kipindi cha kujifungua kitakapofika. Kuwa na mtu anayekupa moyo, na kukumbusha kila mara kukabiliana na kukusaidia kufanya maamuzi wakati uko katika uchungu, inaweza kufanya uzoefu wa kujifungua kwako kuwa chanya zaidi.

Kuna sababu nzuri ya kuwa na msaidizi wakati wa uzazi. Kimsingi, msaidiziwako atakuwa tayari kujifunza kuhusu kujifungua, na kuwa tayari kuacha kila kitu wakati unauhitaji. Hivyo ni muhimu sana kuwa na mipango ya mbele. Kutegemea na ni kituo gani cha afya utajifungulia, msaidizi wako anaweza akaruhusiwa kukaa na wewe wakati wote wa hatua za kujifungua. Ni vyema kuuliza kwa daktari wako kama hili ni jambo ambalo linawezekana kwenye kituo unachotegemea kujifungulia.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.