Ujauzito Wiki ya 21

Jinsi mtoto wako anavyokua katika wiki ya ishirini na moja
Mtoto wako anaongezeka ukubwa tumboni kwako. Kutoka kichwani mpaka kwenye nyayo zake ana urefu wa sentimeta 25.6.

Wiki hii, ute ute mweupe unaoitwa “vermix caseosa” umeanza kumfunika mtoto wako. Hii itatumika kutunza ngozi ya mtoto wako kwa kipindi chote atakachokuwa anaelea kwenye maji ya uzazi “amniotic fluid”.

Unachotakiwa kufahamu kwenye ujauzito wiki ya ishirini na moja
Utakuwa umeshafanya kipimo cha ultrasound mpaka kufikia sasa. Umuhimu wa skani hii ni kuangalia kwamba mtoto anakua na kuendelea vizuri kadiri inavyotegemewa. Mtaalamu wa skani atampima mtoto wako na kuangalia ukuaji na ufanyaji kazi wa viungo vyake upo sawasawa. Pia ataangalia kama mtoto wako ana magonjwa ya tangu tumboni kama mdomo sungura na matatizo ya moyo.
Mtaalamu ataweza kukuonesha uso, mikono, miguu na hata moyo wa mtoto wako kwenye skani. Inawezekana akakupatia pia picha ya kuondoka nayo nyumbani. Hii inategemea na kituo cha afya unachohudhuria. Kama ungependa kujua utapata mtoto wa kiume au wa kike mtaalamu anaweza akakuambia baada ya skani kumalizika.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.