Ujauzito Wiki ya 2

Jinsi mtoto wako anavyoanza kukua katika ujauzito wiki ya pili

Safari ya ujauzito wako huanza pale yai linapoachiwa kutoka moja ya mifuko yako ya mayai (ovari) kuelekea kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes). Hili litatokea wakati fulani mwanzoni mwa wiki hii, mara nyingi karibu na siku ya 14, kama mzunguko wako ni wa siku 28. Yai lako litasubiri kwa kati ya masaa 12 hadi 24 likingojea mbegu liweze kuchavushwa.

Mwenza wako atamwaga karibu mbegu milioni 600 wakati karibu mbegu 200 tu zitafanikiwa kulifikia yai lako. Utatunga mimba iwapo moja ya mbegu hizi itafanikiwa kuupenya ukuta wa nje wa yai lako na kulichavusha.

Yai lako lililochavushwa tayari au “zygote” husafishwa kuelekea kwenye mji wa minba kutokea kwenye mirija yako ya uzazi. Kwa bahati mbaya, kutoka kwa mimba mapema hutokea kwa watu wengi na siyo “zygote” zote hufanikiwa kuwa watoto. Lakini kama ujauzito wako utaendelea vizuri katika miezi tisa ijayo kiumbe hiki kidogo ambacho ni mjumuiko wa seli tuu kitakuwa na kuwa mtoto kamilifu.

Dalili za ujauzito katika wiki ya pili
Japokuwa wewe upo katika hatua za mapema sana za ujauzito, inawezekana ukaanza kuwa na dalili za mimba. Hata hivyo, kila mwanamke ni tofauti. Inaweza kuchukua baadhi ya wanawake muda mrefu kidogo kabla ya kuanza kuhisi kuwa ni wajawazito.

Moja ya ishara za mwanzo unazoweza kuziona ni kupata mchomo au kuwakwa hisia katika matiti yako. Chuchu zako zinaweza kuhisi hisia za maumivu zinapoguswa. Hii ni kwa sababu mimba husababisha kuongezeka kwa usambazaji wa damu katika matiti yako.

Ishara nyingine ya mapema ni badiliko la rangi katika mashavu yako ya uke na uke. Kwa kawaida, uke wako na mashavu ni ya rangi nyekundu mpauko, lakini mimba itasababisha rangi kuwa ya wekundu uliokolea. Hii pia inasababishwa na kuongezeka kwa mzunguko wa damu.

Baadhi ya madoa kwenye nguo ya ndani pia ni ya kawaida. Unaweza kutambua uwepo wa rangi nyekundu mpauko, au rangi ya kahawia katika nguo yako ya ndani , au wakati mwingine maumivu mepesi wakati wa kwenda choo.

Unachotakiwa kufahamu kwenye ujauzito wiki ya pili
Kama unafikiri umeanza kuziona dalili za ujauzito, ni vyema ukafanya vipimo vya mimba (ujauzito). Baadhi ya vipimo vya ujauzito ni vinahusisha namna unavyojisikia, baadhi ya vipimo vinaweza kutambua homoni za mimba mapema kama siku sita baada ya kurutubishwa kwa yai.

Hata hivyo, ishara ya uhakika ya mimba ni kukosa kipindi cha hedhi. Vipimo vya mimba vitakuwa sahihi zaidi kama utachukua kipimo baada ya hedhi yako kutoonekana. Hivyo, inaweza kuwa bora kama utasubiri muda mrefu kidogo kabla ya kuchukua kipimo chako cha kwanza.

Wakati huo huo, unaweza kukuta wewe tayari ni mjamzito. Sasa ni wakati mzuri wa kuanza kula vizuri na kufanya baadhi ya mazoezi mepesi. Kama unavuta sigara ni vyema kuacha sasa.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.