Jinsi ya mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi na saba
Mabadiliko mbali mbali yanatokea katika mfumo wa fahamu wa mtoto wako wiki hii. Aina fulani ya mafuta inayoitwa “myelin” imeanza kuuziba uti wake wa mgongo. Hii itasababisha kuharakishwa kwa taarifa kutoka mwilini kwake kwenda kwenye ubongo.
Usikiaji wa mtoto wako pia unaongezeka. Kama utawasha muziki, anaweza kuonesha kuwa ameusikia kwa kusogea sogea. Unaweza pia ukaanza kumsikia akipiga mateke siku chache zijazo
Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi na saba
Kama ni mara ya kwanza kuwa mjamzito utaanza kusikia kucheza kwa mtoto wako katika kipindi hiki na katika wiki kadhaa zijazo. Hii ni hatua ya kusisimua katika kipindi cha ujauzito.
Unaweza kutambua kwamba mtoto wako ameanza kucheza tumboni mara kadhaa kwa siku. Hisia za kwanza za kucheza huku zinafurahisha au ni kama vipepeo ndani ya tumbo lako. Kwa bahati mbaya, mpenzi wako hana uwezo wa kushuhudia msisimko huu bado . Kwani kupiga mateke hakuanzi mpaka mwezi mmoja ujao na kuendelea.
Wakati mabadiliko haya yote yanaendelea ndani ya mwili wako, unaweza kuona mabadiliko kadhaa juu ya uso wa ngozi yako pia. Miduara mweusi wa ngozi karibu na chuchu zako, iitwayo areola, huongezeka ukubwa na matiti yako kupanuka. Hili ni kawaida kabisa katika kipindi cha ujauzito na inaweza dumu kwa muda mrefu kama miezi 3 baada ya mtoto kuzaliwa.
Mabadiliko mengine ya ngozi hayana madhara kipindi cha ujauzito. Mstari mweusi uitwao “linea nigra” unaweza kujitokeza kuelekea chini katikati ya tumbo lako. Na unaweza kuwa na rangi ya asili nyeusi juu ya uso wako. Maeneo haya ya ngozi nyeusi huisha baada ya mtoto kuzaliwa.
Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya kumi na saba
Bila kujali ni kiasi gani wewe au mwenza wako mnapata kwa mwezi, ukweli utabaki palepale kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi pale mtoto atakapozaliwa. Kama mtaweza kutafuta njia nzuri ya kuhifadhi pesa kuanzia sasa itawasaidia sana hapo baadae.