Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi na sita
Mtoto wako kwa sasa ana ukubwa sawa na parachichi. Mwili wake unaanza kufanya kazi sasa. Mzunguko wa mtoto wako na njia ya mkojo unafanya kazi kikamilifu. Katika wiki chache zijazo atakuwa kwa haraka sana.
Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi na sita
Maumivu ya mgongo, kiuno na mapaja yanakusumbua? Maumivu haya yanaweza kuwa dalili nyingine kipindi cha ujauzito iitwayo “Pelvic Gidle Pain”
PGP hutokea pale homoni ya “relaxin” inalegeza ligamenti kwenye nyonga yako. Kama unapata wakati mgumu kutoka kwenye gari au kukaa na kusimama kwa muda mrefu zungumza na mkunga wako au daktari. Kama hautapata msaada mapema kwa tatizo hili mapema linaweza likaleta shida zaidi kadiri ujauzito wako unavyokua.
Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya kumi na sita
Ni kawaida kabisa kuongezeka uzito wakati wa ujauzito. Kama umeanza na uzito wa kawaida kwa urefu wako (bodymass index) unaweza kuw umeongezeka kati ya 2kg na 4.5kg. Japokuwa ongezeko kubwa la uzito wako huanza kutokea baada ya wiki 20 za ujauzito, uvaaji wa nguo za kubana unaweza ukawa ushaanza kuuchukia.