Jinsi mtoto wako anavyokuwa katika wiki ya kumi na tano
Kuanzia wiki hii mtoto wako ataanza kuzisikia kelele ndani ya mwili wako kama mapigo yako ya moyo na mingurumo ya tumbo lako. Anaweza akaisikia sauti yako lakini itakuwa kwa mbali sana kwa sasa.
Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi na tano
Lakini mabadiliko kwenye rangi, utelezi na harufu ya majimaji haya yanaweza kumaanisha umepata maambukizi ukeni. Maambukizi haya kwa bahati mbaya ni mojawapo ya matatizo kipindi cha ujauzito. Majimaji yenye utelezi mwembamba, rangi ya kijivu na yenye harufu kama shombo ya samaki inamaanisha unaweza ukawa na maambukizi ya bakteria ukeni (bacterial vaginosis). Kama unatokwana ute ute mzito kama maziwa inaweza ikawa una maambukizi ya fangus (thrush). Kama una wasiwasi majimaji ya uke ni ya kawaida au la ni vyema kumuuliza mkunga au daktari wako.
Unachotakiwa kufahamu kwenye ujauzito wiki ya kumi na tano
Unaweza kusaidia ukuaji wa mtoto wako kwa kula mlo kamili wenye uwiano (Balanced Diet).
Jaribu kujumuisha vyakula kutoka kwenye makundi makuu manne ya vyakula; mbogamboga na matunda, vyakula vya wanga kama mkate na wali, vyakula jamii ya maziwa na protini kama nyama, samaki na mayai.