Ujauzito Wiki ya 14

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi na nne
Wiki hii! Mtoto wako ataota nywele kwa wingi mwilini kote, nywele hizi huitwa “lanugo”. Nywele hizi kwa kawaida hutoweka kabla ya kuzaliwa.Misuli ya usoni ya mtoto wako imeanza kufanya kazi. Ameanza kukunja uso na kuweka sura mbalimbali Chini ya kope zake, macho yake pia yameanza kufanya kazi.

Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi na nne
Pengine utakua na hisia kali za kujisikia mwenye furaha kuliko katika miezi mitatu ya kwanza. Unaweza hata ukasahau hali ilivyokuwa mbaya miezi mitatu iliyopita.

Unaweza ukawa na kutokwa na damu puani kwa kipindi cha miezi mitatu ya kati ya ujauzito. Hii ni kwa sababu homoni kwenye mwili wako unaifanya mishipa ya damu kuwa dhoofu. Hii husababisha kama mashimo ya pua yako yatakauka, mishipa yako ya damu inaweza kupasuka. Ukinywa maji mengi na ya kutosha kila siku utaweza kutatua tatizo hili.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya kumi na nne
Sasa ni wakati mzuri wa kufanya mazungumzo na mpenzi wako. Mnaweza kuanza kufikiria juu ya maamuzi ya huduma ya watoto, kama unakusudia kurudi kufanya kazi baada mtoto wako kuzaliwa. Mgawanyo wa majukumu ni muhimu sana katika kipindi cha ujauzito na hata baada ya mtoto kuzaliwa.

Kama uko single/mwenyewe, huu ni wakati mzuri wa kutafuta msaada na kumfahamisha mtu wako wa karibu kuwa wewe ni mjamzito. Unaweza kuuliza wakunga wako kuhusu vikao vya moja kwa moja kabla ya kujifungua, kama hutotaka kwenda madarasa ya wazazi.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.