Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi na moja
Mtoto wako sasa amekamilika kikamilifu, kutoka kichwani mpaka kucha za vidole vya miguu. Ana urefu wa kidole gumba. Vidole vyake vya mikono na miguu vimetengana na baadhi ya mifupa yake imeanza kuwa migumu.
Kwa kipindi cha miezi sita ijayo mtoto wako kazi yake kuu itakuwa kukua zaidi na kuwa na nguvu, tayari kwa ajili ya maisha nje ya mji wa mimba yako (uterus).
Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi na moja
Utakua ukipata wingi wa hisia mpya kimwili sasa kwani wewe ni mjamzito, baadhi ya hisia huridhisha kidogo kuliko nyingine. Kama umeona unavuja mkojo wakati unapiga chafya au kucheka, jaribu kutokuwa na wasiwasi. Kinachosababisha kuvuja huku ni dhiki udhaifu (stress incontinence) na ni kawaida wakati wa ujauzito.
Mara baada ya mimba kutungwa, homoni husababisha tishu na misuli iliyopo kwenye sakafu yako ya nyonga (Pelvic Floor) kunyooka. Hii inaweza kusababisha udhaifu katika misuli (sphincter) ambayo hudhibiti kutolewa kwa mkojo kutoka kibofu cha mkojo.
Wakati unacheka, kukohoa, kupiga chafya au kukimbia, shinikizo ndani ya tumbo lako na kuzunguka kibofu cha mkojo huongezeka. Shinikizo hili hubana kibofu cha mkojo wako. Kwa kawaida, misuli ya sakafu yako ya nyonga husaidia kufunga kwa chini ya kibofu chako cha mkojo. Kama misuli hii ni dhaifu au haiwezi kubana kikamilifu, basi unaweza kupata tatizo kama hilo.
Habari njema ni kwamba kuna hatua unaweza kuchukua ili kuzuia uvujaji. Kufanya mara kwa mara mazoezi ya sakafu ya nyonga itaimarisha misuli inayofanya kazi kudhibiti kibofu cha mkojo. Kaza misuli ya sakafu yako ya nyonga “pelvic floor muscles” kwa sekunde 10– Hii ni ile misuli unayoibana wakati wa kuzuia mkojo au kujizuia usijikojolee pale unapokuwa umebanwa na mkojo. Rudia mara 10 na ni vyema ukafanya kwenye vipindi viwili au vitatu katika masaa 24.
Unachohitaji kufahamu kwenye ujauzito wiki ya kumi na moja
Kati ya wiki hii na wiki ya 14 ya ujauzito wako, utakuwa unafanyiwa skani ya “ultrasound”. Sababu kuu ya Scan hii ni kujua una ujauzito wa wiki ngapi, na kukadiria tarehe yako ya kujifungua kutokana na kipimo cha “ultrasound” pia kuangalia maendeleo ya mtoto wako na kuonyesha kama unatarajia mapacha, utatu au zaidi.
Unaweza kuacha kutumia virutubisho vya foliki asidi (folic acid) kutoka mwishoni mwa wiki hii, kwa sababu kiunganishi taarifa (neural tube) cha mtoto wako kitakuwa kimeshaundwa kikamilifu.