Ujauzito Wiki ya 10

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi
Moyo wa mtoto wako mpaka sasa umeshajengeka kikamilifu. Unapiga karibia mara 180 kwa dakika. Mtoto wako sasa rasmi ni kijusi. Yeye yupo katika nafasi ya ukuaji na ataongezeka ukubwa zaidi maradufu katika kipindi cha wiki tatu zijayo. Mtoto wako sasa anameza na anapiga mateke, na viungo vyake vyote vikuu ni vikamilifu. Vitu vidogo vidogo vinaanza kuonekana pia, kama vile kucha na vinyweleo vidogo vya nywele juu ya kichwa chake.
Viungo vya uzazi vya mtoto wako (sehemu za siri) vimeanza kuonekana. Katika skani ya ujauzito wako, ambayo inapaswa kufanyika hivi karibuni, unaweza kuwa na uwezo wa kujua kama wewe unatarajia kupata mtoto wa kiume au wa kike.

Dalili za ujauzito katika wiki ya kumi
Unaweza kuwa umeanza kuona kwamba kiuno chako kinatanuka, ingawaje pengine huna haja ya kununua nguo kubwa kubwa kwa muda huu.
Kadiri mtoto wako anavyokuwa, mji wa mimba yako (kizazi) kinapanuka kwa ajili ya malazi yake. Mfuko wa uzazi wako kwa sasa una ukubwa sawa na kifungu cha zabibu (Grapefruit), karibu na ukubwa wa kutosha kujaza nyonga (pelvis) yako. Unaweza hata kuwa na uwezo wa kuhisi mji wa mimba yako kwa juu na katikati ya mfupa wako wa nyonga (pubic bone). Sehemu hii ipo chini ya kitovu.

Pengine bado unahisi kichefuchefu, umechoka, au kusikia kichwa kizito. Jikumbushe mwenyewe ni raha kiasi gani kuwa unatarajia kuleta kiumbe duniani. Hii inaweza kusaidia kukupa furaha wakati wa huzuni.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya kumi
Hivi sasa, unapaswa kukutana kwa mara ya kwanza na mkunga (daktari) wako, katika miadi (appointment) uliyopangiwa. Kutakuwa na mengi ya kukamilisha katika miadi (appointment) hizi za kwanza. Orodhesha maswali yote ambayo ungependa kupata majibu kutoka kwa daktari au mkunga wako na hivyo kupata majibu bora ya muda wako na mkunga (daktari).
Pamoja na skani yako ya kwanza, unaweza kuwa na vipimo vingine ili kuona jinsi mtoto wako anavyokua na kuongezeka. Kutegemea na hospitali utakayoenda unaweza ukafanyiwa skani kati ya wiki 11 pamoja na 13. Pia baada ya wiki 13 unaweza kufanyiwa kipimo cha kugundua kama mtoto atapata ugonjwa wa utindio wa ubongo (Down syndrome) kwa wale wanaoishi sehemu ambazo kipimo hiki ni kawaida kufanyika

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.