Anemia(upungufu wa seli nyekundu za damu kwenye damu) baada ya kujifungua ni ugonjwa wa muda mrefu unasobabishwa na upungufu wa madini ya chuma baada ya kujifungua.
Kuna hatua tatu za anemia:
Hatua ya kwanza
Hakuna dalili zozote zinazoonekana katika hatua hii, kiwango cha chuma ndani ya uboho wa mfupa kinapotea na kusababisha kupungua kiwango cha chuma ndani ya damu.
Hatua ya pili
Athari za anemia zinaanza kuonekana. Kichwa kuuma na kusikia kuchoka ni dalili mojawapo. Upungufu wa madini unaweza kuonekana baada ya kipimo cha damu kufanyika. Katika hatua hii uzalishaji wa haemoglobini unaanza kuathiriwa.
Hatua ya tatu
Viwango vya haemoglobini (protini nyekundu iliyo na madini ya chuma, inayosafirisha oksijeni ndani ya viumbe hai) vinapungua, na kusababisha athari za anemia kuongezeka. Kuchoka sana na uchovu ni dalili kuu katika hatua hii, zinazosababisha kuumwa.
Chanzo cha Anemia baada ya kujifungua
- Mlo hafifu: ulaji haba wa madini ya chuma kabla na bada ya ujauzito unaweza kusababisha anemia baada ya kujifungua. Madini ya chuma yanayohitajika mwilini wakati wa ujauzito ni 4.4 mg kwa siku. Kwa kuwa madini ya chuma kwenye chakula hayatoshi, ni muhimu kutumia virutubisho vya madini chuma wakati wa ujauzito na kabla ya kupata ujauzito. Upoteaji wa damu kipindi cha hedhi inaweza kusababisha upungufu wa madini ya chuma mwilini kabla ya kupata ujauzito.
- Upotevu wa damu nyingi wakati wa kujifungua inasababisha upungufu wa madini yaliyotunzwa mwilini na kupelekea anemia naada ya kujifungua. Upotevu wa damu nyingi unaongeza hatari za mama kupata anemia.
- Magonjwa ya tumbo la chakula, kama uvimbe yanaongeza ufyonzaji wa madini ya chuma kwa wingi.
Dalili za Anemia baada ya Kujifungua
Zifuatazo ni baadhi ya anemia zinazoonyesha upungufu wa madini ya chuma baada ya kujifungua:
- Kuchoka na kujisikia mchovu.
- Ngozi kupauka.
- Kuwa mnyonge.
- Kupungua wingi na ubora wa maziwa ya mama,inayopelekea uzito wa watoto kupungua.
- Kichwa kuuma.
- Moyo kwenda mbio.
- Kupungua hamu ya tendo la ndoa.
- Upungufu wa kinga ya mwili.
Hatari zinazoletwa na Anemia baada ya Kujifungua
Anemia inaweza kuleta hatari kwa mama ikiwa tiba haitapatikana kwa muda:
- Kushindwa kumaliza kazi za kila siku kwasababu ya kuchoka na uchovu
- Kushindwa kutulia na kufanya kazi.
- Ongezeko la nafasi ya kuzaa mtoto njiti au kupata shida wakati wa kujifungua, mimba zijazo.
- Kufariki ghafla kwasababu ya athari kubwa ya kizunguzungu na uchovu.
Wanawake walio katika makundi yafuatayo wana hatari ya kupata Anemia baada ya kujifungua:
- Upungufu wa madini ya chuma kabla na wakati wa ujauzito.
- Ujauzito wa mapacha au zaidi.
- Uzito wa BMI zaidi ya 24
- Kujifungua kwa njia ya upasuaji
- Kupata ujauzito mwingine baada ya mda mfupi tangu mimba ya mwisho.
- Kutoka damu wakati wa ujauzito.
- Kujifungua kabla ya muda.
- Shinikizo kubwa la damu kipindi cha ujauzito
- Plasenta previa- ni tatizo ambapo plasenta inashindwa kusogea kwenda juu hivyo inakuwa chini karibu kabisa na mlango wa kizazi.
- Kipato kidogo
Anemia inaathiri unyonyeshaji?
Ndio. Anemia inahusiana na tatizo la kukosa maziwa ya kutosha, ambayo inapunguza unyonyeshaji wa kutosha wa mtoto na kupelekea mtoto kuachishwa kunyonya mapema
Mtoto kuachishwa kunyonya mapema kunafanya uzito duni kwa mtoto. Matibabu ya anemia mapema yanazuia matatizo ya unyonyeshaji.
Jinsi Anemia baada ya kujifungua inavyotibiwa
Matibabu ya anemia baada ya kujifungua inajumuisha mabadiliko ya mlo na maisha yako. Vifuatavyo ni vidokezo 11 vya kukusaidia:
- Tumia virutubisho vya madini ya chuma, kuimarisha viwango vya madini chuma kwenye damu.
- Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi navyo ni kama: mboga za kijani kama spinachi, maharage,boga, nafaka, mchele wa kahawia, viazi,nyama, kuku,matunda kama strawberi na vyakula vingine vya asili.
- Punguza matumizi ya chai, chai ina “tannin” inayopunguza kasi ya madini ya chuma kufyonzwa ndani ya mwili. Pia ulaji wa ya vyakula vyenye kalsiamu unapunguza kasi ya ufyonzaji wa madini ya chuma ndani ya mwili.
- Kula vyakula vyenye vitamin C vitakusaidia kuongeza ufyonzaji wa madini chuma ndani ya mwili. Matunda kama machungwa na strawberi ni vyanzo vizuri.
- Kunywa vimiminika zaidi ili mwili wako uwe na maji ya kutosha itayosaidia kuimarisha usambaaji wa damu baada ya kujifungua. Vimiminika kama maji vinasaidia kupunguza damu kuganda na maambukizi ya kibofu cha mkojo (UTI). Kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku. Maji yanasaidia kulainisha kinyesi na kuzuia kukosa choo.
- Pata mapumziko ya kutosha
- Maambukizi ya mwili yataongezeka ikiwa kinga ya mwili itapungua. Madini ya chuma yanapopungua mwilini, onana na daktari mapema kupata antibaiotiki.
- Muone daktari mapema kama umepata anemia baada ya kujifungua. Fanya vipimo vya damu itamsaidia daktari kujua hali yako na kuchukua hatua stahiki.