Kwanini naoneka kama bado nina ujauzito?
Itachukua muda mwili wako kurudia hali yake ya awali, haswa tumbo lako baada ya ujauzito.Umeshajifungua lakini utaonekana kama bado una ujauzito wa miezi sita, ndani ya tumbo lililobonyea-bonyea na kubwa.
Ili kuelewa zaidi, chukulia tumbo lako kama pulizo linalojaa kadiri mtoto anavyokua tumboni. Kujifungua hakumaanishi pulizo linapasuka ila linaanza kuisha upepo taratibu. Kupungua kwa ukubwa wa tumbo lako kunaweza chukua mda lakini kutafanikiwa.
Tangu mtoto anapozaliwa,mabadiliko ya homoni yatasababisha tumbo lako lipungue ukubwa. Itachukua karibu wiki nne kwa mfuko wa uzazii kujibana na kurudia hali yake ya kawaida.
Seli za mwili zilizojazwa wakati wa ujauzito zitaanza kutolewa nje ya mwili kwa mfumo wa mkojo, uchafu ukeni, jasho. Na mafuta ya mwili ya ziada yataanza kupungua kwaajili ya kumlishia mtoto,yataanza kuunguzwa, hususani kama unanyonyesha na kufanya mazoezi. Itachukua angalau wiki kadhaa kuona matokeo. Baada ya kujifungua mstari mweusi uliopo tumboni ujulikanao kama “linea nigra” bado utaonekana pamoja na michirizi.
Mstari huu (linea nigra) unasababishwa na rangi ndani ya ngozi ambapo misuli ya tumbo lako imevutwa na kuachanishwa, ili mtoto apate nafasi ya kuishi kadiri anavyoendelea kukua. Mstari huu unapotea miezi michache baada ya kujifungua.
Michirizi inasababishwa na kunyooshwa kwa ngozi ya tumboni kumudu ukuaji wa haraka wa mwili wako kipindi cha ujauzito. Michirizi hii inaweza kuwepo kwenye tumbo,makalio,mapaja na matiti.
Je, itachukua mda gani tumbo langu kurudia hali yake ya awali?
Tumesikia stori nyingi za wanamama wapya waliorudia miili yao ya awali ndani ya wiki chache. Japokuwa inawezekana lakini haitokei kwa wamama wote. Kumbuka! Mwili wako unaweza badilika umbile lake baada ya ujauzito. Inaweza kuwa ngumu kurudia umbile lako na uzito wako wa awali.
Uvumilivu ndio ufunguo. Ilichukua miezi tisa misuli ya tumbo lako kunyooka ili kumudu mtoto mzima ndani yake. Hivyo ni sawa kuchukua muda na muda zaidi kukaza tena katika hali yake ya awali.
Kasi na digrii ya kukaza kwa tumbo kunategemea yafuatayo:
- Umbile na ukubwa gani uliokua nao kabla ya kubeba mimba
- Kiasi gani cha uzito uliongezeka wakati wa ujauzito
- Unafanya kazi kiasi gani
- Jeni (gene) zako ulizorithi
Utagundua kupoteza uzito ni rahisi kama;
- Uliongezeka chini ya 13kg na ulifanya mazoezi mara kwa mara wakati wa ujauzito.
- Kama unanyonyesha
- Mtoto wako wa kwanza.
Unaweza kurudia uzito wako wa awali mpaka miezi sita baada ya mtoto kuzaliwa.
Nawezaje kupungua uzito na kufanya tumbo langu kuwa na muonekano mzuri?
Kunyonyesha inasaidia, hasa miezi ya kwanza baada ya kujifungua. Ikiwa unanyonyesha, utaunguza kalori za ziada zitakazo tengeneza maziwa –karibu 500 kwa siku. Unaweza kupoteza uzito mapema zaidi ya wamama wanaonyonyesha kwa chupa.
Kunyonyesha kunasababisha kubana misuli ya tumbo, na kuufanyisha mwili mzima mazoezi. Lakini kama unakula zaidi ya kuufanyisha mwili mazoezi ili kuunguza mafuta mwillini, utaongezeka uzito, hata kama unanyonyesha.
Ni sawa kupungua uzito wakati wa kunyonyesha. Mwili wako una ufanisi katika kutengeneza maziwa, na kupungua mpaka kilo 1 kwa wiki ambayo haina athari kwenye wingi wa maziwa unayotengeneza.
Walakini, kama una mtoto mdogo wa kuangalia unahitaji nguvu nyingi. Jaribu kupungua uzito baada ya kutoka kujifungua inaweza kuchelewesha kupona na kukufanya uhisi kuchoka zaidi. Na ni vema zaidi kuacha kujipunguza (diet). Subiri mpaka uchunguzi wa baada ya kujifungua utakapofanyika kabla ya kujaribu kupungua uzito.
Kula kwa afya, pamoja na mazoezi laini itakusaidia kurudia umbile lako. Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vitakavyokusaidia kutunza uzito wenye afya:
- Tenga muda wa kula kifungua kinywa.
- Kula angalau sehemu tano ya matunda na mbogamboga.
- Jumuisha vyakula vingi vyenye nyuzinyuzi (fiber) vitakavyosaidia usafirishaji wa chakula, kama vile shayiri, maharage, nafaka, mbegumbegu na mbogamboga.
- Jumuisha vyakula vya ngano kama mkate, mchele, pasta au viazi kwenye milo yako.
- Punguza vyakula vyenye fati nyingi na sukari kama biskuti na keki.
Nifanye nini kingine niweze kurudia tumbo langu la awali kabla ya ujauzito?
Mazoezi yanaweza kusaidi kukaza misuli ya tumboni na kuunguza kalori. Ikiwa ulikua unafanya mazoezi kipindi cha ujauzito mpaka mwisho unaweza kuanza kufanya mazoezi mepesi na kujinyoosha tangu mwanzo.
Kama uliacha kufanya mazoezi wakati wa ujauzito au wewe ni mgeni kwenye mazoezi ni vizuri ukaanza mazoezi taratibu zaidi.
Wamama wapya wanaweza kuanza na mazoezi ya sakafu ya nyonga na kufanyia kazi taratibu kupunguza tumbo la chini mara baada ya kujisikia wako tayari. Hii inaweza kukusadia kurudia umbile lako la awali na kupunguza tumbo.
Unaweza kumbeba mwanao na kuenda matembezi kidogo, hii itasaidia kuinua hisia na kufanya mazoezi mepesi ya mwili wako.