Tatizo la Mtoto Kukosa Choo

Nitajuaje mwanangu wa mwaka mmoja mpaka mitano anakosa choo?

Katika suala la kujisaidia haja kubwa hakuna kinyesi cha kawaida au ratiba ya wakati wa kujisaidia. Cha muhimu ni kipi cha kawaida kwa mwanao. Anaweza akajisaidia kila baada ya kula au baada ya siku moja au zaidi. Watoto wa miaka minne wanajisaidia mara tatu kwa siku na mara tatu kwa wiki.

Kwa kuangalia kinyesi cha mwanao, itakusaidia kujua kama mwanao anapata shida ya choo. Ishara hizo ni kama zifuatazo.

  • Kinyesi kikubwa na kigumu kinachompatia shida wakati wa kujisaidia.
  • Kinyesi kidogo na kigumu kinachofanana na mavi ya mbuzi

Tabia ya mwanao itabadilika na kukujulisha pia. Watoto wenye shida ya choo wana:

  • Jisaidia haja kubwa mara chache zaidi
  • Onyesha ishara za kubana kinyesi, wakati mwingine kusimama na vidole vya mguu.
  • Lalamika tumbo kuuma au kuvimbiwa.
  • Sumbua sana.
  • Poteza hamu ya kula.

Kwanini mtoto wangu anakosa choo?

Ni hali ya kawaida watoto kukosa choo wanapoanza kujifunza kujisaidia wenyewe au wanapoanza shule.

Sababu za kukosa choo kwa watoto ni pamoja na;

  • Kukosa maji na vyakula vya nyuzinyuzi vya kutosha (fibre).
  • Inahusiana na maswala ya kujifunza kujisaidia
  • Msongo wa mawazo au wasiwasi.

Jinsi ya kutibu hali hii.

Onana na daktari mapema kama una wasiwasi mwanao anakosa choo. Kabla ya kumuona daktari unaweza jaribu mambo kadhaa ili kutuliza hali hii:

  • Ongeza ulaji wa matunda na mbogamboga kwa mtoto wako, bila kusahau vyakula ambavyo ni vyanzo vizuri vya nyuzinyuzi (fibre) kama matunda, mboga za majani, maharage na nafaka nzima. Matunda kama tofaa (apple),zabibu, peasi na strawberi.
  • Mhamasishe kunywa maji mengi anagalau glasi sita kwa siku. Inaweza kuwa maji, maziwa au juisi,ili kufanya kinyesi cha mtoto kuwa laini.
  • Mazoezi ya viungo kama kutembea, kupanda na kukimbia kila siku yanasaidia.
  • “Massage” tumbo la mwanao
  • Usimharakishe mtoto kujifunza kujisaidia mwenyewe kama hayuko tayari. Kumlazimisha inaweza kumfanya aogope au awe na wasiwasi unaopelekea mtoto kubana haja kubwa.
  • Watoto wanaokosa choo, mara nyingi hawajui wakati gani wa kujisaidia. Msaidie mwanao kwa kumuhimiza kukaa chooni dakika 10 baada ya kula, au kabla ya kwenda kulala. Utulivu wa mtoto wakati wa kujisaidia unamsaidia mtoto kujisaidia vizuri,hakikisha unamuwekea midoli na michezo karibu na poti lake wakati akijaribu kujisaidia.
  • Zawadi baada ya kujisaidia ni motisha nzuri kwa mwanao ikiwa anabana haja kwasababu ya woga.
  • Ikiwa mwanao anaenda shule hakikisha unajua kama anajisaidia shuleni vizuri. Watoto wengine ni wagumu kujisaida hasa wakiwa mbali na nyumbani.

Vidokezo hivi vinaweza kumsaidia mwanao, ni muhimu kumuona daktari wako pia. Itachukua mda mrefu mtoto kurudia hali ya kawaida kujisaidia akikosa choo kwa muda mrefu.

Wakati huu jaribu kutulia, kukosa choo kwa watoto inaweza kuwa hali ngumu kupambana nayo hasa mwanao anapochafua nguo zake za ndani kila mara. Mpatie usikivu wako na hakikisha una nguo nyingi safi. Tiba sahihi itamsaidia mtoto kurudia hali yake ya awali.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.