Muda Gani Mtoto Anaanza Kuota Meno

Kumbuka huu ni muongozo tu, watoto wote wanatofautiana wakati wa kuota meno. Ni jambo la kawaida kabisa mtoto kuota meno yake mapema kabisa yaani ndani ya miezi minne au kuchelelwa mpaka miezi 15. Watoto wachache wanaweza kuzaliwa na meno! Kumbuka watoto waliozaliwa kabla ya muda au wenye uzito duni wanaweza kuchukua mda mrefu kuota meno.

Mwezi Mtoto Mchanga
Miezi 5(kawaida miezi 4-7) Meno yanaanza. Fizi za mtoto wako zinavimba na kuwa nyekundu, meno mapya yanaanza kuchomoza. Baadhi ya watoto wanaumia meno yakianza kuota na wengine hawaumii, lakini watoto hawatulii kiujumla. Mkumbatie na kumfariji sana.
Miezi 6( kawaida miezi 5-10) Meno ya kwanza ya mwanao yanaota, mara nyingi meno mawili ya katikati chini (lower central incisors). Ujio wa meno haya utamfanya mwanao kupunguza usumbufu na maumivu.

 

Miezi 7( kawaida miezi 6-12) Meno ya juu ya katikati (the upper central incisors) yanaanza kuota wakati huu.

 

Miezi 9-16( kawaida miezi 9-12) Meno ya juu upande wa kulia kutokea katikati (the upper lateral incisors) yanaanza kuchomoza. Meno ya chini upande wa kulia kutoka katikat ( lower lateral incisors) yanafuata.
  Mtoto mkubwa
Miezi 14( kawaida miezi 12-19)

 

Magego ya kwanza yanaanza kuota upande wa chini na juu wakati mmoja. Magego ni meno yaliyo nyuma katika kinywa cha mtoto yanayotumika kusaga na kuponda chakula.

 

Miezi 18 ( kawaida miezi 16-23) Meno ya pembeni-chonge juu na chini ya kinywa yanaanza, meno haya yanatumika kurarua na kuchana chakula.

 

Miezi 26( kwaida 20-33) Magego ya pili yanaanza kukua juu na chini kwenye fizi.
Miaka miwili na nusu-miaka mitatu Mtoto wako ana meno timilifu ya kwanza 20
Miaka minne Taya na mifupa ya uso inakua na kuruhusu meno ya awali kutoka na meno ya utu uzima kuchukua nafasi. Kung’oa meno ya kwanza kwa mtoto kunaanza wakati huu. Kawaida watoto wa kike wanang’oa meno yao ya kwanza kabla ya watoto wa kiume, mara nyingi ni jino la chini la kwanza linang’olewa.

 

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.