Mtoto Wiki ya 7

Jinsi mtoto wako anavyokua

Mtoto wako kapoteza muonekano wake wa kitoto na kaanza kuonekana kama mtu mdogo! Anaonekana mwenye kasi zaidi na kuchukua tahadhari mara umwinuapo wima.

Mara mtoto anapokua amelalia tumbo lake, anaweza kunyanyua kichwa na kifua chake kwa muda, akionekana kama anapiga push-up ndogondogo. Hii inamsaidia kudhibiti kichwa chake,maana ni hatua ya ukuaji wake.

Muunganiko kati ya wewe na mtoto wako unakua kila siku inapopita. Ukizungumza anaweza kuacha anakoangalia na kukutazama wewe, au kuacha kula na kukusikiliza wewe. Endelea kuongea nae, rudia minong’ono na kelele zake.

Elezea unachofanya ukiwa unatembea ndani ya nyumba, na msomee mtoto wako kila uwezapo. Unapomsomea mtoto haikupi tu furaha na hali ya kuridhika, ila pia inasaidia kukuza lugha ya mtoto.

Maisha yako: kutafuta huduma ya haki ya watoto

Kama una mpango wa kurudi kazini, aidha ndani ya mwezi au mwaka, si mapema kufikiria kuhusu huduma za watoto. Ni vema kuwatafuta mmfanyakazi wa ndani mzuri mapema kwa ajili ya kuhudumua watoto.

Unaweza ukawa una urahisi zaidi kama utaamua kumtumia dada wa kazi.kama una mpango wa kufanya kazi nyumbani itabidi ujipange vizuri ili uweze kupata muda wa kutosha kufanya kazi zako.

Kwa sasa utakua umefanikiwa kukutana na wakina mama wengine ambao wana watoto wadogo kama wewe, hapa unaweza kubadilishana mawazo na wenzako na kupata mawazo mapya.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.