Mtoto Wiki ya 6

Jinsi mtoto wako anavyokua

Tangu pindi mtoto amezaliwa, mtoto wako amekua akikua zaidi na kuwa karibu zaidi na wewe au mwenzi wako. Kwa sasa anaweza weka hadharani kuwa nyinyi ndio watu wake awapendao, kwa kunong’ona na kupiga mateke kwa furaha kila akikuona. Na kila unapozidi kumkumbatia, kumtekenya, kucheza nae inakupa fursa zaidi ya kuona tabasamu lake la kwanza mapema.

Mtoto wako anakua nyeti sana kwa mazangira yaliyomzunguka. Kwa mfano, unaweza gundua jinsi anavyokabiliana na kelele za ghafla kama kengele ya mlangoni. Anaweza kuruka, kulia au kukaa kimya akiwa anajaribu kuelewa hisia mpya ya kushangaza.

Kuna uwezekano kwamba mtoto wako akapendelea sana sauti yako na ya mwenzi wako. Tengeneza nafasi kuongea, kumsomea au kupiga kelele azipendazo zaidi.

Hata kama mtoto wako hakuelewi unachozungumza, kumpa nafasi kusikia sauti yako ni msingi mkuu wa kujifunza kuongea baadae. Haijalishi ni maneno gani unayotumia. Unaweza kunyooshea kidole vitu vilivyo karibu na kuelezea rangi na maumbo, na kutoa maelezo ya haraka ya kile unachokifanya au kuongea kuhusu familia na marafiki.

Maisha yako: vipimo vyako baada ya ujauzito

Muda fulani baada ya wiki chache mbeleni,daktari wako au mtaalamu wako wa afya atatoa nafasi ya vipimo baada ya ujauzito, kuhakikisha wewe na mtoto wako mnaendelea vizuri. Kama una maswali au hoja, au una tatizo kukabiliana na hali ya kuwa mama mwenye mtoto mdogo, huu ndio wakati mzuri wa kuliongelea na mtaalamu wako.

Wamama wengi huhisi kuzidiwa, hasa wakiwa wanakumbwa na msongo wa mawazo baada ya ujauzito. Mtaalamu wako wa afya atakua tayari kukusaidia na pia unaweza kumtafuta wakati wowote.

Mtaalamu wako anaweza pia kutoa uchunguzi wa kimwili kuhakikisha kua unapona vizuri. Unaweza pia kuongea nae kuhusu lishe, ili kuwa na uhakika kuwa hauna upungufu wa madini chuma. Anaweza pia kutaja uwezekano wa njia za uzazi wa mpango na kukusaidia kuchagua njia nzuri kwako kutumia.

Kama unahisi uko tayari kwa tendo la ndoa tena, itakua vema kujaribu kabla ya vipimo vyako baada ya ujauzito. Kwa njia hii, kama utapata hali isiyo ya kuridhisha, utafanikiwa kulisema wakati uko kwenye kituo cha afya. Ila hakuna haja ya kuharakisha hili tendo. Endelea na mazoezi ya sakafu ya nyonga, haya yatasaidia tendo la ndoa kuwa la kuridhisha wakati uko tayari kujaribu tena.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.