Mtoto Wiki ya 3

Jinsi mtoto wako anavyokua

Inaweza kukuwia vigumu kuamini, ila tayari mtoto wako ana karibia umri wa mwezi mmoja! Unaweza kumwona mtoto akijaribu kunyanyua kichwa chake ukiwa umemlaza kwenye tumbo lako. Mwishoni mwa wiki anaweza kufanikiwa, na pengine kuweza kugeuza kichwa chake upande mmoja kwenda mwingine. Unaweza pia kugundua miguu na mikono yake kupunguza kusogea kwa kasi na sio kwa kushtuka shtuka kadiri anavyoendelea kupata uwezo wa kuitumia misuli yake.

Mtoto wako bado hana utaratibu maalumu wa kulala. Lakini unaweza kuanza kumfundisha kuhusu tofauti ya usiku na mchana. Kadiri anavyokua, utaratibu wake wa kulala utaanza kuwa na mpangilio maalumu.

Maisha yako: Kukabiliana na ukosefu wa usingizi

Katika kipindi hiki utagundua ya kwamba tatizo la kukosa usingizi linakuandama sana. Kujisikia mwenye uchovu mwingi na wakati mwingine kuongea maneno yenye kukatika katika bila kumalizia sentesi. Hali hii ni tatizo kwa wanawake wengi wiki za mwanzo baada ya kujifungua. Jaribu kulala au kupumzika kila mtoto wako anapolala. Ni vyema kuacha kila kitu kwa muda na kupata muda wa kupumzika.

Jaribu kuwa na mawazo chanya. Kuongea na wazazi wengine wenye watoto wakubwa inaweza kusaidia. Wameshayapitia haya na watakuwa tayari kusaidia mbinu mbalimbali za kupambana na uchovu. Ni vyema pia kuzungumza na mtaalamu wako wa afya kuweza kujua kama unapata madini chuma ya kutosha.

Kuwa na uchovu kunaweza kukupa wakati mgumu kukabilia na mtoto pindi akiwa analia. Wakati mwingine yaweza onekana kama mtoto analia kila wakati. Kujua sababu zinazomfanya mtoto analia inaweza kukusaidia kukabiliana na tatizo kiurahisi.

Mtembele mtaalamu wa afya kwa sana. Ongea nae au mtaalamu wa unyonyeshaji kama unapata matatizo yeyote kipindi cha kumnyonyesha mtoto. Maziwa kuwa mengi, titi kuuma, chuchu kupasuka na maambukizi kwenye titi ni baadhi ya matatizo ya kawaida kwa mama anayenyonyesha, ila upo msaada wa kutosha kwa matatizo hayo.

Kila kitu kinaweza onekana ni cha kuchosha sana kwa sasa ila hali ya kawaida itarudi hivi karibuni katika familia yako.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.