Mtoto wako anavyokuwa
Katika wiki ya pili, mtoto wako anaanza kuwa na nguvu kila siku kwa kufanya mazoezi ya kunyonya, kushika na kupepesa macho wakati wa kutafuta chuchu.
Mara nyingine anaweza akakushika jicho na kukuangalia. Huo huwa muda muafaka kumwangalia pia kwa makini na kutabasamu huku ukiongea nae. Kuangaliana macho na mtoto ni njia mojawapo ya kuanzisha ukaribu nae.
Watoto wako tofauti, kuna ambao hutulia zaidi ya wengine. Lakini kama mwanao analia kwa muda mrefu sana, hiyo inaweza kuwa dalili ya maumivu ya tumbo (Colic). Wataalamu hawana uhakika ni watoto wangapi wanapata hayo matatizo (Colic), ingawa inadhaniwa kati ya asilimia tano na ishirini hupata madhara hayo katika kipindi fulani.
Kama mtoto wako atapata hayo matatizo (Colic), utakuwa na kipindi kigumu kwa wiki chache, ingawa kuna mengi unaweza kufanya katika kipindi hicho.