Wiki ya kwanza ya miezi 14
Jinsi mwanao anavyokua.
Mwanao anajifunza mambo mapya kila kukicha, kuanzia kuaga kwa kupungia, na kunywa kwa kutumia kikombe. Ingawa bado hajajifunza tabia nzuri mezani
Katika umri huu, kula ni kitu cha kujifunza, kujifunza lazima kuchafuka huku na kule
Mpatie kijiko au uma kisha mwachie mwanao ajifunze kwa namna yake mwenyewe, na unaweza kumvua nguo ya juu ili kupunguzakuchafua nguo.
Unaweza kupata vitu vya kukataza papo hapo na vitu vya kumkubalia mwanao mara moja na kumpongeza haswa kipindi hichi cha utoto, hakikisha kwamba ngazi zimelindwa na makabati ya chini yamefungwa na vitu vya kuvunjika vimetolewa maeneo yanayofikika kirahisi
Miezi 14 wiki ya 2
Jinsi mwanao anavyokua
Je mwanao ameanza kuwa mwoga wa vitu, ambavyo havikumsumbua mwanzoni, kama vile mashine ya kufulia, mashine ya kusafishia ndani, au mbwa, woga wa mwanao utaanza kupotea anavyokuwa na imani ya kutosha.
Kama bafuni ni eneo la kutisha kwa mwanao sasa jaribu kumwogesha na kitaulo au kitambaa laini. Mwache akae bafuni na umwagie maji taratibu bila kutumia kikombe.
Jaribu kupunguza muda wa kuoga kwa mwanao, na kuleta midoli mipya ya kuoga nayo ndani ya maji, au ukaamua kuoga nae ili kumfanya asiwe mwoga tena
Miezi 14 wiki ya 3
Jinsi mwanao anavyokua
Kama mwanao anawashwa na kuvuta sikio, inaweza kuwa ishara ya maambukizi ya sikio.
Mpigie daktari wako kama utahisi mwanao ana maambukizi ya sikio, lakini usitarajie kupewa dawa papo hapo hivyo daktria wako atakushauri usubiri siku mbili ama tatu kabla ya kumpatia mtoto dawa.
Kama ni hali ya hewa mwanao anaweza kuacha midoli yake ya zamani mara tu kitu kipya kinapokuja machoni mwake ili kuepuka usumbufu kuwa na boksi la midoli kila chumba atakachokuwepo mwanao.
Mshirikishe mwanao katika kusafisha na kuondoa midoli baada ya kucheza, na usitegemee afanye peke yake wakati huu. Unaleta wazo hilo kwa ajili ya baadae, fanya kiwe kitu cha furaha kwa kuimba au kuweka wimbo wakati wa kufanya usafi.
Miezi 14 wiki ya nne
Jinsi mwanao anavyokua
Mwanao anakuza uwezo wake wa kuongea kila wakati sasa. Na neno lake analolipenda “hapana” usichukie anajifunza tu.
Usichukie kama mwanao hajaanza kufanya mambo ya ambayo watoto wengine wameshafanikiwa kufanya. Kumbuka watoto hutofautiana na baadhi hufanya mambo kwa haraka na wengine huchelewa.