Mtoto Mwaka 1

Jinsi mtoto wako anavyokua

Heri ya siku ya kuzaliwa, mtoto wangu! Mwaka wako wa kwanza tangu uzaliwe umeisha na maisha ya utotoni yako nyuma yako. Miezi ijayo, mtoto wako atapendelea kujitegemea zaidi, na kugundua dunia katika upande mzuri, kujua uchangamfu wake, na mengine mazuri, jifunze kusema nakupenda.

Maisha yako: kurahisisha woga wa kumuacha

Japo mtoto wako anaanza kugundua uhuru wake, bado ana wasiwasi wakati unaondoka. Hii ni hali ya kawaida. Kurahisisha kuondoka kwako, ruhusu muda mwingi wa kuwa nae. Mtaarifu msaidizi wako kuwasili mapema kabla haujaondoka ili kumpa mtoto wakati wa kuzoea.

Usimtoroke au kumuaga kwa mda mrefu, fanya haraka kwa kumpatia busu moja. Kama utamsikilizia mtoto wako kwa nje, utagundua mtoto wako kupunguza kulua mara ukitoka mbele ya macho yake. Ni ngumu kutojisikia hatia, ila unamsaidia mtoto wako kujitegemea kwa kutokua nae mda wote.

Ficha baadhi ya midoli
Ni wazo zuri kuweka mbali midoli yote mipya na kuitoa mara chache, ili mtoto wako asielemewe. Unahitaji kutengeneza mahali pa kuhifadhi midoli, ili kuweka vipande vidogo vidogo vya midoli ya mtoto kuchezea. Unaweza kutumia maboksi ya viatu,makopo ya biskuti na maboksi ya zawadi kwaajili ya kuhifadhia midoli ya mtoto wako.

Ishara kwa mtoto
Katika mwaka wa pili, watoto wengi wanasumbuliwa na kushindwa kusema mahitaji yao, japo wanajua wanachokitaka ila hawana ujuzi wa lugha wa kusema. Ishara za watoto imekua ni mbinu mpya. Wewe na mtoto wako mnaweza kujifunza ishara nyingi na kusaidia kukuambia akitaka chakula zaidi au anahitaji kinywaji. Baadhi ya watu wana wasiwasi matumizi ya hizi ishara yanaweza kuchelewesha kuongea kwa mtoto lakini imekua kinyume.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.