Jinsi mtoto wako anavyokua
Katika umri huu,mtoto wako ana uwezekano wa kuanza kutambaa. Kama bado hajaanza usiwe na shaka. Baadhi ya watoto wanachukua muda mrefu kidogo, na wengine wanapendelea kuzunguka kwa kujivutavuta kwa makalio yao au tumbo mpaka watakapo kuwa tayari kuamka na kutembea.
Kwa sasa mtoto wako anaweza kuanza kuwa na mizunguko zaidi,haitachukua mda kabla hajaanza kujigonga au kuanguka. Bila kujali ni kwa kiasi gani uko makini, kuna mambo ambayo hayaepukiki hasa anapojifunza kutembea.
Moyo wako unaweza kushtuka kidogo, ila sasa ni wakati wa kufurahia kumwangalia akichunguza mazingira yanayomzunguka na kugundua mipaka yake.
Kumruhusu mtoto wako kuchunguza mazingira yanayomzunguka kutampatia nafasi ya kucheza kwa ubunifu na kujifunza mengi kuhusu dunia. Kwa shiyo hakikisha kutengeneza mazingira mazingira salama kwa mtoto wako nyumbani. Kwa njia hiyo itakufanya kusikia bila wasiwasi akiendelea kuchunguza.
Njia nzuri ya kuhakikisha nyumba yako ni salama kwa mtoto wako, ni kwa kutambaa mwenyewe kwenye sakafu. Kwa kufanya hivi kunaweza kukusaidia kugundua chochote ambacho kitakua hatari kwa mtoto. Ondoa kitu chochote cha kupasuka, sukuma televisheni yako nyuma, na okoa samani yoyote kwenye ukuta ili kuepusha kudondoka.
Maisha yako: Muda wa wanandoa
Baadhi ya wazazi wapya wanasema mara ile hali ya mtoto kuwa mgeni katika familia kupotea, wanaanza kuwa mbali kati ya mmoja na mwingine. Ni hali ya kawaida kama badiliko kama hili linaweka doa katika mahusiano yenu. Kitu cha muhimu ni kuendelea kuzungumza pamoja na kueleza jinsi wote mnavyojisikia.
Kama mwenzi wako anafanya zaidi huduma ya mtoto, jaribu kuelewa ni kwa kiasi gani ni kazi ngumu, na ni kiasi gani unaweza kujisikia kutengwa kwa baadhi ya mida. Na kama wewe ndo unayekaa na mtoto wako muda mwingi, elewa kwamba mwenza wako anaweza kujisikia mpweke, na kukosa mda wa kipekee na wewe.