Mtoto Miezi 7

Jinsi mtoto wako anavyokua

Mtoto wako bado hana misuli ya kutosha kuweza kushika kijiko lakini inawezekana anajaribu hivyo hivyo kujilisha mwenyewe. Pengine anakataa kulishwa na wewe, au anachukua chakula kutoka kwenye sahani yako. Japokuwa hii inaweza ikakuudhi lakini ni dalili muhimu inayoonesha uwezo wa mtoto wako kujitegemea.

Jaribu kumuwekea vyakula vya kushikika na mkono wake mdogo na uone namna anavyojaribu kuweka mdomoni na kula. Pamoja na kwamba hana meno, bado anaweza kufurahia vyakula vya aina mbalimbali.

Wazazi wengi wanaogopa kukabwa pale watoto wao wanapoanza vyakula vigumu. Ni vyema kuwa makini na kuwa karibu na mtoto wako mda wowote ule ambao atakuwa anakula.

Maisha yako: Umerudi kazini?

Kama likizo yako ya uzazi imekaribia kuisha, unaweza ukawa umeshaanza kuwaza kuhusu kurudi kazini. Kama ndivyo unaweza ukawa unajihisi mwenye hatia kumuacha mtoto wako uende kazini. Au unaweza ukawa una hamu ya kurudi kazini na unajisikia mwenye hatia kutokujisikia mwenye hatia kumuacha mtoto wako.

Kama utaendelea kubaki nyumbani inawezekana ukawa unajisikia una hamu ya kwenda kazini. Unaweza pia ukawa unasikia wivu kwa watu wengine wanaoenda kazini. Isipokuwa kama unaishi kwenye eneo lililojitenga, kutengeneza urafiki na wazazi wapya ni rahisi sana. Wazazi wengine vile vile watakuwa na hamu ya kutengeneza urafiki na wewe.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.