Jinsi mtoto wako anavyokua
Mtoto wako anaendelea kujifunza zaidi jinsi ya kuzionesha hisia zake, hivyo unaweza kuanza kuona mabadiliko kwenye muonekano wa uso wake na namna anavyoitikia uwepo wako. Ana uwezo wa kukufanya uelewe kuwa ana hasira, amechoshwa au mwenye furaha. Na uwezo wako wa kuonesha upendo umeanza kujijenga.
Kama una bahati unaweza ukapata makumbatio na mabusu kutoka kwa mtoto wako. Lakini ana uwezo mkubwa wa kuonesha mapenzi kwako kwa kukuangalia machoni na kuliwazwa na harufu yako. Anaweza akacheka kwa vioja vidogo vidogo, na kujitahidi kukufanya ucheke pia. Endelea kumfanya acheke kwa kutoa nyuso tofauti tofauti na milio mbali mbali.
Kinga ya mwili ya mtoto wako bado inajijenga, na anaweza akapata maambukizi mbali mbali katika mwaka wake wa kwanza. Ni kawaida kuwa na wasiwasi mtoto wako anapokuwa na tumbo la kuvuruga, upele au homa. Hizi ni mojawapo ya hatua tuu za ukuaji.
Jifunze kutambua namna unavyoweza kutambua mtoto wao ana dalili za homa ili uweze kutambua pale atakapokuwa anahitaji msaada wa daktari.
Maisha yako: Ngono baada ya kujifungua
Inawezekana upo tayari kimwili kuanza kufanya ngono tena. Ila inaweza ikawa ngumu kupata muda na nguvu pia. Hizi ni baadhi ya njia unaweza kutumia kurudisha matamanio ya kimapenzi.
Kutaniana:
Utani kidogo na mpenzi wako unaweza kurudisha mambo vizuri. Sio lazima hat amuwe kwenye chumba kimoja. Kutumiana ujumbe wa maneno wa kimapenzi mkiwa mpo mbali pia husaidia.
Pangilia vizuri:
Kupanga mda wa kufanya mapenzi inaweza isionekane kama ni jambo la kimahaba. Lakini kuandaa mtu atakayekuwa anaangalia mtoto wenu wakati nyote wawili hampo kwa masaa machache ni muhimu. Ndugu au jamaa anaweza akawa wa msaada pia. Ila sio lazima ajue mnakwenda kufanya nini mpaka mmeamua kumuachia mtoto. Kama itawezekana pia mnaweza mkajiiba na kufanya kitendo kimoja kitamu na cha haraka wakati mtoto amesinzia.
Furahieni usiku mmoja pamoja:
Sio lazima mtoke mmevalia na kwenda nje usiku ili muweze kufurahia mapenzi yenu. Mnaweza mkafanyiana massage (kukandana) na pia kuoga pamoja wakati mtoto wenu amelala. Hii pia inaweza kuzirudisha hisia zako za ngono kwa haraka.
Kuwa mcheshi:
Kuwa tayari kwa lolote. Kama unanyonyesha maziwa yanaweza kuanza kutoka na kutiririka wakati mkifanya ngono, hivyo kuwa na taulo karibu. Kama mtoto wako ataanza kulia, subiri kwa dakika chache kuona kama atarudi kulala mwenyewe. Kama itabidi muahirishe ili uweze kumuhudumia mtoto wako, usikate tamaa na kuacha usiku huu. Anzeni upya kwa taratibu na matayarisho ya kuchezeana vya kutosha muone nini kitatokea.