Jinsi mtoto wako anavyokua
Ukuaji wa mtoto wako ni wa kasi, na kuwa na nguvu kila siku. Uwezo wa kukidhibiti kichwa chake unaendelea kukua, na anaweza kukinyanyua kichwa chake juu kwa sekunde chache akiwa anashangaa dunia inayomzunguka.
Unaweza ukagundua mtoto wako anashangazwa bila kutarajia na mikono yake mwenyewe. Bado hajaweza kuelewa kwamba ni moja ya kiungo cha mwili wake, na anaweza kuidhibiti, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kupata uwezo wa kufikia vitu na kufahamu mambo.
Kinga ya chanjo kwa mtoto wako ni ndani ya mwezi huu, na inakulazimu kuwa na maswali kama, ni aina gani ya chanjo? Itatolewa lini? Ni nini kitatokea kwenye hiyo siku? Je mwanao anaweza kupata chanjo kama anamafua au anakohoa?.
Pengine unaweza ukawa na wasiwasi kuhusu mtoto wako kupata chanjo ya sindano. Ni hali ya kawaida kuwa na wasiwasi na unaweza kushangaa kama ni salama kwa mtoto kupatiwa kinga.
Maisha yako: Jinsi ya kuwa mzazi jasiri
Kwa sasa umefikia hatua ya kuweza kukabiliana na ukuaji wa mtoto wako ingawa sio kazi nyepesi, umeweza kujua hisia na mahitaji ya mtoto wako pia, inaonekana unajitahidi kupambana na hali ya kuwa mzazi.
Jitahidi kupata usingizi wa kutosha kipindi mtoto amelala mchana. Kama una mtoto mkubwa pia, jaribu kumwomba rafiki au ndugu kumwangalia wakati unapumzika.
Mara nyingine unaweza kugundua kwamba kuwa mzazi kunachosha. Kulisha, kubadilisha nepi na kuogesha mtoto imekua mambo yanayochukua mda mwingi wa siku yako. Habari njema ni kwamba mtoto wako anakua, pongezi kwa jitihada, na unaweza kuzawadiwa sauti za kitoto, minong’ono ya mtoto wako na tabasamu zuri kutoka kwa mwanao.