Mtoto Miezi 11

Jinsi mtoto wako anavyokua

Juhudi zote kuongea, kuimba na kumsomea mtoto wako zinaanza kulipa sasa. Kama bado hajasema neno lake la kwanza,haitachukua mda. Jitaharishe kuingia katika ulimwengu mpya wa kuwasiliana na mtoto wako.

Ubongo wa mtoto wako bado unaendelea kukua kwa kasi ya ajabu, ukiruhusu habari nyingi. Hakikisha kuendelea kuongea nae kadiri uwezavyo, elezea dunia inaokuzunguka kwa undani zaidi.

Hata kama hausikii maneno unayoyajua, unaweza gundua mtoto wako anatumia aina Fulani ya sauti kutaja vitu anavyovipenda.

Pindi mtoto atakapoanza kupiga kelele za sauti, msikilize kwa ukaribu, na mjibu sauti anazozifanya. Atapenda kuzungumza na wewe, kwahiyo ongea nae pia, na msubiri akujibu. Anaposema kitu kinachosikika kama neno la ukweli, lirudie kwake, na muonyeshe jinsi ya kulisema vizuri.

Mtoto wako anaelewa maneno mengi zaidi anavyoweza kusema, na ujuzi katika lugha yake unaendelea kuimarika kila mda. Jitahidi kurudia maneno mara nyingi ili apate nafasi ya kushika maana ya maneno. Kadiri anavyoendelea kusikia maneno katika umri mdogo ni bora zaidi.

Maisha yako: Kutokubaliana kuhusu nidhamu

Kwa sasa, utu wa mtoto utaanza kuonezakana vizuri, hasa akiwa anajifunza kujielezea uamuzi wake. Huu ni wakati wa kufurahisha, ukiwa unacheza na kuongea na mtoto wako inakua furaha zaidi. Ila pia ina maanisha atakua na maoni yake mwenyewe katika kile anachotaka kufanya, ambacho kitakua tofauti na malengo yako.

Kujitegemea kupya kwa mtoto wako kunaweza kuonyesha maoni tofauti kati ya wewe na mpenzi wako kuhusu jinsi gani ya kumsimamia tabia yake. Mnaweza kuwa na maoni tofauti juu ya malezi ya watoto. Hata hivyo, kawaida hakuna jibu baya au zuri, cha msingi ni kutafuta ni jambo gani ni zuri kwa mtoto.

Jaribu kuheshimiana na kupendezwa na maoni ya mwenzako, japo inaweza kuwa ngumu muda fulani. Ukweli ni kwamba kutokubaliana kwa jambo mara nyingi, huonyesha jinsi mnajali maendeleo ya mtoto.

Kama hamjafanikiwa kukubaliana jambo, ni vema kusema na kusikika kuliko kukosoana au kumezea jambo. Jaribu kuwa mkweli kuhusu wasiwasi wako huku ukijua kwamba mwenzi wako ana matarajio mema kwa mtoto wako. Kama mazungumzo yatakua ya utata sana na hamuelewani, jaribu kuchukua dakika tano kupumzika, alafu rudi na kuangalia kama mnaweza kupata maelewano juu ya hili swala.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.