Mtoto Miaka 4 na Mwezi 1 – (Miezi 49)

Jinsi mtoto wako anavyokua.

“Moja, mbili”, tatu”, mtoto wako anasema akiwa anapanga vitu vyake vya kuchezea. Na mpaka sasa, inawezekana anajua namba ya mwisho atakayofikia ndio kiwango cha vitu vya kuchezea aluvyonavyo. Kitu ambacho anaweza asiwe anajua kwa sasa ni kwamba hata ukivipangilia tofauti vitu vyake vya kuchezea akivihesabu kwa mara nyingine idadi yake itakuwa ile ile. Unaweza ukavipanga mbali mbali zaidi na ukamuuliza akuambie idadi yake. Anaweza akakuambia ana vitu vinne vya kuchezea badala ya vitatu kwa sababu sasa  hivi vipo mbali mbali zaidi.

 

Watoto wanaokaribia kuanza shule wanaelewa kuhusu idadi kulingana na muonekano wa vitu husika. Kama kifurushi kimoja cha vitu vya kuchezea ni kirefu kuliko kingine wataamini kina idadi ya vitu vingi kuliko kile kifurushi kifupi. Hataweza kuwa na uelewa kwamba urefu wa kifurushi sio lazima umaanishe wingi wa vitu ila inawezekana ni vitu vichache ila ni vikubwa zaidi. Hii ni kwa sababu wanazingatia zaidi muonekano wa vitu kuliko uelewa wa idadi, ambao ni uwezo mkubwa zaidi kwa umri wake.

 

Majina ya watoto yana umuhimu sana kwao. Kwa uhalisia jina la mtoto wako inawezekana ndio neno la kwanza atakalojifunza na kulisoma. Wakati fulani akishafikisha umri wa miaka minne anaweza kuanza kuonesha nia ya kuliandika jina lake pia. Wakati fulani ataanza kutambua kuwa baadhi ya herufi zinahusika na jina lake au ni “herufi zake”. Msaidie kwa kuliandika jina lake kwa herufi kubwa na zinazoonekana kwenye karatasi kubwa. Muache afuatilie kwa kidole au kalamu mkitamka kila herufi kwa sauti pamoja.

 

Maisha yako wakati huu

Sikukuu ya kuzaliwa ya mtoto wako iliyopita inaweza ikawa imesababisha kuongezeka kwa midoli au vitu vya kuchezea vya mtoto wako kwenye nyumba. Ni wakati wa kuanza kupunguza na kupanga vitu vya mtoto wako vya kuchezea. Unaweza ukavipunguza na kuondoa vile vitu ambavyo amechoka kuvichezea au alikuwa anavichezea akiwa na umri mdogo zaidi na kuviweka stoo au kuvitupa kama vimechakaa sana. Wakati mwingine unaweza pia ukavigawa kwa ndugu, jamaa au rafiki wenye mtoto mwenye umri husika wa vifaa unavyotaka kupunguza. Ukumbuke kuwa kama utamuuliza mtoto wako kama anahitaji bado kuendelea kuchezea au kutumia kifaa fulani, bado atasema ndiyo kwani ni vigumu sana kwa watoto kuruhusu kutupwa au kuchukuliwa kwa vitu vyao.

 

Inashauriwa pia kama mtoto ana vitu vingi vya kuchezea ni bora kuficha baadhi ya vitu na kuwa unavitoa na kumpa achezee kila baada ya muda fulani. Mtoto mwenye vitu vingi sana vya kuchezea kwa wakati mmoja inamnyima mtoto umakini wa kutulia na kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu. Kuwa na vitu vichache vya kuchezea kunaleta uelewa wa upangiliaji na inapunguza wasiwasi kwako na kwa mtoto wako.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.