Mtoto Miaka 4 na Miezi 2 – (Miezi 50)

Jinsi mtoto wako anavyokua

“Ninaweza kufanya mwenyewe!” mtoto wako anakuambia wakati unamvalisha nguo asubuhi (au wakati anapiga meno mswaki, akisaidia kupanga meza, au ukifanya chochote). Kadiri uwezo wa mtoto wako wa kimota unavyokua, anaweza akawa anasukuma mikono yako mbali kadiri unapotaka kumsaidia kufanya jambo kwani anataka kufanya kila kutu mwenyewe. Hii inaweza kukufanya ukose uvumilivu wa kusubiri, lakini inashauriwa usimuingilie mtoto wako mapema na kutoa msaada kwani yupo kwenye hatua muhimu za mwanzo za kujifunza vitu mbali mbali na kujitegemea.

Katika miaka minne mtoto wako anatakiwa awe anaweza kuvaa nguo mwenyewe, japokuwa anaweza bado akawa anasumbuliwa na zipu na vifungo. Kurahisisha na kumfundisha hatua hii haraka jaribu kuchanganya na kumpa pia nguo ambazo ni rahisi kuvaa, kama suruali zenye mpira wa kuvutika kiunoni au viatu vya kudumbukiza.

Kitu kimojawapo ambacho lazima uendelee kuwa unamsimamia ni wakati wa kupiga meno mswaki. Mtoto wa miaka minne bado hajawa na muungano mzuri wa matendo kuweza kusafisha meno yake kwa ufanisi. Muache asafishe mwenyewe kwa muda halafu uingilie kati na kumsaidia kumalizia hatua za mwisho.

Maisha yako wakati huu.

Hakikisha familia yako yote inatenga muda kwa ajili ya kupata kifungua kinywa. Ni mlo muhimu kuliko milo yote ya siku lakini ndio mlo ambao haupewi kipaumbele. Sababu zinaweza kuwa labda wazazi wapo na majukumu mengi na watoto kutoamka wakiwa na njaa.

Ulaji wa kifungua kinywa ni muhimu sana kwa mtoto wako kwani ubongo utahitaji chakula baada ya kuwa umelala usiku kucha. Hii itamsaidia mtoto wako pia kuwa na usikivu, tabia nzuri na pia kuwa na maendeleo mazuri shuleni bila kusahau kupungua kwa uwezekano wa kupata unene uliopindukia. Utajisikia vizuri na kuwa na uwezo wa kula bora zaidi katika siku kama ukila kifungua kinywa vizuri asubuhi.

Unaweza ukaandaa chakula cha asubuhi kwa ajili ya kifungua kinywa tangu usiku mmoja kabla, ili kupunguza ugumu wa kuandaa kila kitu asubuhi husika.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.