Mtoto Miaka 3 na Miezi 9 – (Miezi 45)

Jinsi mtoto wanavyokua

Je,kuna sauti nzuri kama mtoto wako akiwa anacheka? Ni sauti nzuri hasa kama wewe ndo unamchekesha. Watoto wa miaka mitatu wanapenda vichekesho vinavyoonekana. Ni wakati mzuri wa kufanya vituko vichache kumfanya mwanao acheke. Kwa mfano unaweza kuvaa sweta lako nje ndani au kuvaa viatu mikononi. Vitu vya kutokea bila kujua vinaweza mfanya acheke zaidi.

Vitu vya kijinga vinaweza kuwa njia ya kumfundisha mtoto, chukua herufi au namba zipange kwa makosa anaweza kukucheka kwa ujinga wako huo, na kuanza kuzipanga vizuri kama anazifahamu. Yote haya yakiwa yanaendelea mwanao atakua mwenye kucheka sana hii ni nzuri kwake.

Ikiwa mwanao hawezi kuruka, kukimbia au kusimama na mguu mmoja,usijali. Mfumo wa kuratibu mwili wa mtoto unatofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine. Baadhi ya watoto wako tayari kujaribu tangu awali wakati wengine wanapendelea kukaa pembeni na kuangalia mpaka wakiwa tayari kufanya jambo kubwa.

Maisha yako sasa

Kwa wazazi wengi desturi ya kuchukua kumbukumbu za picha za mtoto alipokua mdogo ilikua kubwa,ila kadiri anavyokua hali ile inapungua. Utagundua kuwa kumbukumbu nzuri za mwanao sio picha zilizopigwa vizuri na kuwekwa ukutani, ila matukio ya kila mda na siku. Hivyo basi weka simu au kamera karibu na wewe mda wowote uwe tayari kuchukua kumbukumbu ya tukio fulani ikiwa ni bafuni, wakati wa kulala, wakati wa kula au hata wakati wa kucheza.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.