Jinsi mtoto anavyokua
Maswali mengi yanakuja hasa mwanao anapokaribia miaka minne. Maswali kama ni sawa yeye kutumia kompyuta? Kuna siku ambayo hatakunywa uji?
Simu za kupapasa au kompyuta zinaweza kuwa njia nzuri za kujifunza lakini pia sio nyenzo za lazima katika umri huu. Kama mwanao anapendelea na yuko tayari kujifunza kupitia kompyuta na simu tafuta michezo mizuri na “app” za simu (Ubongo Kids – Akili na mimi) zenye michezo ya watoto kukuza ubunifu wake au hesabu na kusoma,kuhesabu,kuzitambua herufi na kuimba pia.
Maisha yako sasa
Nyumba yako kupangiliwa ni vigumu hasa kama unakaa na mtoto mdogo wa miaka mitatu, unaweza kuchanganyikiwa ukifikiria unadhifu wa nyumba sasa. Unaweza panga nyumba yako na muda huohuo mwanao kuvuruga. Polepole mwanao ataweza kurudisha midoli yake kwenye boksi na vitu mahali alipovikuta baada ya kutumia, lakini ni baada ya kuanza kwenda shule.