Jinsi mtoto wako anavyokua
Mchakato wa mwanao kujifunza kutofautisha ukweli na ndoto ni wa polepole. Mwaka huu utakua mwaka wa kuvutia kwake kwasababu kila anachowaza kichwani kwake anajua ni ukweli. Ataanza kutoa majukumu kwa vifaa au watu ambapo haiwezekani ila kwa mwanao ni sawa. Mtoto wako ataamini barua zinapaa kutoka kwa aliyetuma mpaka nyumbani. Atafikiri anaweza ongea na ndege na kuna binadamu kwenye mwezi. Itachukua muda mwanao kugundua kuwa vitu vingi anavyofikiria sio vya ukweli mpaka miaka nane.
Maisha yako sasa
Una shida wakati wa kulala? Ratiba yako ya kulala imeharibiwa kwa miaka miwili iliyopita, ni vizuri kuandaa na kurudisha mazingira na tabia nzuri ya kulala. Kwanza hakikisha chumba chako kina giza, hakikisha hakuna komputa au televisheni chumbani kwako(wataalamu wa mambo ya usingizi wanashauri hivyo). Kuna mambo mengi ya kufanya baada ya mwanao kulala kama kuangalia mitandao ya kijamii au kuangalia televisheni, usipoteze muda mwingi kukimbizana nayo, kumbuka mwanao anaamka mapema sana hivyo ni vizuri kulala mapema ili uamke na nguvu nyingi.