Mtoto Miaka 3 na Miezi 5 – (Miezi 41)

Jinsi mtoto anavyokua

Una sababu nzuri ya kujivunia na mwanao mwenye miaka mitati na miezi sita sasa. Uwezo wake wa kusaidia kazi ndogondogo, kukuza lugha yake na mawazo vinaimarika pia, muda huu atajitahidi kuandika jina lake mwenyewe.

Inafurahisha kuanza kuona herufi zinaumbika vizuri. Kuandika ni moja ya hatua ya ukuaji inayotofautiana mtoto mmoja na mwingine. Hivyo, ondoa shaka kama mwanao hana hamu ya kuandika.

Unaweza kumuhamasisha kwa kuweka chaki au karatasi na penseli mahali anapoweza kufikia. Pia unaweza tumia sukari au unga wakati mkiwa jikoni na kuweka kwenye sinia, kasha muonyeshe jinsi ya kuunda maneno.

Watoto katika umri huu wanagundua na kuiga sauti mbalimbali wanazozisikia kutoka kwako au baba yake, au katuni wanazoangalia. Utaweza kumuona akiongea na midoli yake huku akiiga tukio aliloliona hapo awali. Pia mtoto anaweza kugundua kuwa watu wazima wanaongea tofauti kulingana na mtu anayeongea nae, anaweza gundua kuwa unaongea tofauti pale unapoongea na mama yako na unaoongea tofauti unapozungumza na mwajiri wako.

Maisha yako sasa

Baadhi ya wakati hata wazazi wazuri,wenye subira,wacheshi,wanataka kupiga kelele! Kumlea mtoto kunachosha hasa pale usingizi unapokua finyu. Jaribu kutoka na kufanya manunuzi,kutembea mwenyewe ,sikiliza muziki unaopenda.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.