Jinsi mwanao anavyokua
Mwanao anaweza kukuaibisha kwa maswali atakayokuwa anakuuliza hasa mbele za watu. Ni wakati mzuri wa kufanya maongezi nae kuhusu mambo kama miaka,jinsia,rangi ya mtu au ulemavu.
Mfano mnatembea barabarani na mwanao na kisha akamuona mtu mwenye mguu mlemavu na kukuuliza kwa sauti, “mama mwangalie yule mtu na mguu wake” wewe kama mzazi mfanye aelewe kuwa ni hali ya kawaida na kwanini amekua vile alivyo kwa kuyafanya maelezo kuwa mafupi. Unaweza muelezea kuwa “mtu yule alipata ajali na kupoteza mguu wake, lakini madaktari watampatia mguu mpya” maelezo kama haya yatakua rahisi kwa mtoto wa miaka mitatu kuelewa.
Ili kukuza uwezo wa mwanao kuongea, hadithi ni njia nzuri ya kumsaidia. Msomee au mwadithie hadithi mbalimbali sasa.
Maisha yako sasa
Ni mwaka mzuri wa kusikia maneno ya kufurahisha au misamiati mipya kutoka kwa mwanao, unaweza kuandika kwenye kitabu na itakuwa na umuhimu hapo badae.
Je, mwanao anakupuuzia? Utapata matokeo mazuri ya tabia ya mwanao kama ukitumia lugha nzuri na mwanao. Mfano badala ya kumwambia “twende tukaoge”, unaweza sema “weka midoli yako pembeni mwanangu sasa ni muda wa kuoga, mtoto mzuri”