Jinsi mtoto wako anavyokua
Ni muda muzuri wa kumpiga picha mwanao au kuchukua video na kulinganisha jinsi gani amekua na jinsi gani amekuwa jasiri. Utagundua amekua mrefu na miguu yake imekua membamba. Watoto wa miaka mitatu wanaanza kupungua unene wao wa utotoni.
Ni wakati mzuri wa kuanza utaratibu wa kunawa mikono, kwasababu mwanao anashika vitu vingi na vingine sio salama kwa afya yake, pia mara nyingi anaweza kuweka mikono yake mdomoni. Pia kwasababu ameanza kutumia choo mwenyewe ni vizuri utaratibu huu kuanzishwa.
Unaweza kumsaidia mwanao kukuza ustadi wa kutumia mikono yake vizuri kwa kujumuika nae katika shughuli kama:
- Kupika- mruhusu achanganye vitu kwa kutumia mwiko au kijiko.
- Kufanya kazi bustanini kwa kutumia jembe
- Kutumia zana za mziki kama ngoma,kinanda cha watoto
Maisha yako sasa
Je, unataka mwao akusikilize? Jaribu kumnong’oneza mwanao. Unaweza kufikiria kumuongelesha mwanao kwa sauti kubwa kunaweza kusaidia, la hasha! Kumuongelesha mwanao kwa sauti kubwa kuna muogopesha au atakupuuzia kama umekua ukifanya mara nyingi. Kumnong’oneza au kuongea nae kwa sauti ya chini kwa upande mwingine kutamfurahisha mwanao, mwanao atajishusha na kutaka kusikiliza maneno unayomwambia. Watoto katika miaka hii wanavutiwa na vitu kama siri,kitu cha kipekee au chochote kitakachopendekeza jambo zuri au la kufurahisha linakaribia kutokea.