Jinsi mtoto anavyokua
Zawadi nzuri unayoweza mpatia mwanao sasa hivi, ni boksi kubwa au chocho kitakachokusidia kutengeneza gari, nyumba au roketi. Inaweza sisimua ujuzi,hisia na ustadi zidi ya midoli ya kieletroniki.
Kucheza kwa kuigiza (kimama-mama, kidaktari au kipolisi) kunafanyika sana mtoto akiwa na miaka mitatu.
Watoto wanajifunza kwa kuwaza na kufanya. Wanapoigiza kuwa polisi au mzazi wanapata uhuru wa kuchunguza kasi ulimwengu wanaoishi. Wanakua na mamlaka. Wanaweza elezea hisia, wanajifunza kujadiliana na kutatua matatizo(kama jinsi gani ya kupika au kuwakamata watu wabaya). Wanajifunza kuelewa matatizo ya watu na kuwaonea huruma.
Maisha yako sasa
Kuwa karibu na mtoto wa miaka mitatu sio jambo la mchezo. Pale mambo yanapokua mengi na kuchanganyikiwa jaribu kupumua, pumua kwanguvu ndani kisha hesabu mpaka tano, bana pumzi yako na hesabu mpaka saba alafu pumua taratibu kwa kuhesabu mpaka nane. Rudia mara nne au tano(funga macho kama unaweza), taratibu utatulia.