Jinsi mtoto anavyokua
Mtoto ana miaka mitatu tangu kuzaliwa sasa, mwanao anazidi kujitegemea na kukua vizuri kila siku. Anaweza kuandaa chombo cha chakula kwa ajili yake. Pia anaweza kujivalisha nguo na kuchagua aina ya rangi zinazoendana katika nguo zake. Pia anaweza kutembea, kusimama, kukimbia na kuruka.
Maisha yako: mlo wa familia
Mlo wa pamoja na familia ni jambo muhimu kwa sasa. Kukaa pamoja mezani na kumfundisha mtoto tabia za mezani kama vile jinsi ya kukaa mezani, kusikiliza, ushirikiano na mawasiliano. Kama hamuwezi kukaa kwa pamoja kila siku, panga ratiba nzuri kwa ajili ya mtoto japo mara moja au mbili kwa wiki.
Mpango wa siku ya kuzaliwa.
Kuna uwezekano mtoto anajua anachohitaji na atakachopata kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa, Ikiwa umepanga kumfanyia sherehe jaribu kumuhusisha katika maandalizi. Jaribu kumshawishi kuchora au kuandika jina lake au barua ya kushukuru ikiwa atataka.