Jinsi mtoto anavyokua
Mtoto wako amebobea katika kutembea sasa. Hatua zake ni nyingi zaidi na anakaribia miondoko ya kiutu uzima sasa. Pia ameimarika katika michezo ya viungo kama vile kukimbia na kurusha mpira.
Pia ana uwezo zaidi wa kujiangalia mwenyewe. Ataweza kusafisha meno yake mwenyewe ingawa bado anahitaji msaada wako..
Msaidie kusafisha na kukausha mikono yake mbele ya sinki ili kumuonyesha hatua zote zitakazomsaidia kujifunza katika kufungua na kufunga. Sabuni ya kipande itamfaa zaidi kwa mikono yake midogo kuitumia kuliko ile yamaji. Uwezo wake wa kufikiri unaendelea kukua hivyo bado atahitaji msaada wako wakati mwingine.
Utagundua kuwa mtoto wako sasa anaendelea kukua kwa kuchukulia uangalizi baadhi ya vitu na kufanya vitu vingi yeye mwenyewe, kama vile kupanda katika kiti cha gari na kukusanya midoli yake mwenyewe.