Mtoto Miaka 2 na Miezi 8 – (Miezi 32)

Jinsi mtoto anavyokua

Kama ambavo mwanao anaendelea kutambua watu na kutengeneza maada kutokana na anayezungumza naye. Ataanza kutumia maneno tofauti tofauti katika sauti ya kitoto kuwasiliana na watoto na wakubwa. Na utagundua kuwa anatumia lugha rahisi.

Mtoto wako ataanza kufanya baadhi ya vitu mwenyewe na hatapenda kuingiliwa, na utagundua ni ngumu kumkatisha anachokifanya. Mfano, anaweza kumwaga maji msalani baada ya kujisaidia au kusafisha mikono yake baada ya kutoka chooni, yote hii anajaribu kujitegemea mwenyewe.

Unaweza kumsisitiza mtoto kutumia choo kama wewe na wengine mnavofanya, muonyeshe poti linalobeba kinyesi chake unapoenda kutupa na hapo atagundua wapi anatakiwa  kwenda. Tengeneza choo kwa namna ya kumfanya mtoto awe huru kwa kumuwekea stuli ya miguu au kiti kwa sababu ya usalama wa mwanao.

Programu ya AfyaTrack

Programu ya kwanza nchini Tanzania ya kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto kwa lugha ya Kiswahili.